KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, February 4, 2010

Hatma ya shangaziye Obama kujulikana

Shangaziye rais Barrack Obama wa Marekani mzaliwa wa Kenya, Zeituni Onyango, kwa mara ya pili hii leo atajaribu kuwasilisha ombi lake la kutafuta hifadhi ya kisiasa nchini Marekani.
Ombi la kwanza lilikataliwa na serikali ya nchi hiyo mwaka wa 2004 na alihitajika kurejeshwa nchini Kenya. Tangu wakati huo amekuwa akiishi Marekani bila kibali.

Kesi ya Bi Zeituni, ilipata umaarufu zaidi mwaka wa 2008, wakati wa kampeini ya uchaguzi wa urais. Rais Obama, alinukuliwa kusema kwamba hakujua shangaziye alikuwa akiishi nchini humo, bila idhini. Na rais Obama amesema sheria ni sharti ifuate mkondo wake.

Jaji mmoja nchini Marekani alitupilia mbali amri ya kutimuliwa kwa Bi Zeituni Onyango, na badala yake kuanzisha kesi itakayosilikiza ombi lake la kutaka hifadhi ya kisiasa

No comments:

Post a Comment