Kiongozi wa chama cha upinzani cha United Democratic Forces nchini Rwanda, Ingabire Victoire Umuhoza ameshambuliwa na kundi la vijana alipokuwa kwenye tarafa moja mjini Kigali kwa ajili ya kupata kitambulisho.
Bi Ingabire alirejea nchini humo hivi karibuni akitokea uhamishoni kwa lengo la kugombea kiti cha urais katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Mwandishi wetu Yves Bucyana alimkuta Bi Ingabire katika hospitali ya Mfalme Faycal ambaye hakupata maumivu yeyote.
Amemweleza kuwa vijana hao walimnyang'anya begi lililokuwa na vitambulisho vyake na kumwuumiza mfuasi wake Joseph Ntawangundi aliyejaribu kuingilia kati.
Bi Ingabire aliyetangaza kugombea kiti cha urais amekilaumu chama tawala kuhusika na shambulio hilo
No comments:
Post a Comment