KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Maharamia wakamata meli ya Korea


Jeshi la majini la Umoja wa Ulaya limesema meli iliyobeba kemikali na mabaharia 28 kutoka Korea ya Kaskazini imetekwa na maharamia karibu na Somalia.
Meli hiyo ya MV Theresa VIII, linalosimamiwa na Singapore lilitekwa nchini Somalia, maili kadhaa kaskazini magharibi mwa Seychelles.

Jeshi hilo limesema meli hiyo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Mombasa nchini Kenya, lakini ikageuza safari yake kwenda kaskazini.

Jeshi la majini la Umoja huo, Navfor linafanya shughuli zake eneo hilo kulinda meli hizo.

No comments:

Post a Comment