KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Dhahabu yazidi kunufaisha waasi Kongo


Makundi ya waasi wanaokiuka vikwazo yanatorosha takriban tani 40 za dhahabu kila mwaka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa Umoja wa Mataifa ameieleza BBC.
Dino Mahtani amesema kiasi kikubwa cha dhahabu kinadhibitiwa na makundi ya waasi wanaotumia mapato hayo kununulia silaha.

Bw Mahtani, ambaye anatarajiwa kuwasilisha taarifa mbele ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki hii, alisema: "Fedha hizi zinawasaidia kujitosheleza [makundi ya waasi] katika maeneo yao.



"Kiasi kikubwa cha dhahabu kinasafirishwa kwenda Dubai kupitia Uganda," aliongeza.

Bw Mahtani, ambaye ni mratibu wa vikwazo vya silaha wa Umoja wa Mataifa, ameieleza BBC kuwa: "Hivi karibuni kulikuwa na ripoti ya baraza la seneti la Kongo ambalo lilieleza kuwa kwa makadirio dhahabu yenye thamani ya dola bilioni moja nukta mbili ($1.24bn) au tani 40 zinatoroshwa nje ya nchi kila mwaka bila kupitia forodha.

No comments:

Post a Comment