Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameyashutumu mataifa ya magharibi kwa kupinga sera zake.
Amesema mataifa hayo yalipinga sera zake za ugawanyaji ardhi ili Zimbabwe itegemee chakula kutoka nje. Hayo ameyasema katika kikao cha viongozi cha Umoja wa Mataifa kuhusu chakula mjini Roma.
Rais Mugabe amesema sera mbovu zinazoshinikizwa na mataifa yenye uwezo zinaifanya nchi yake kuwa masikini.
Pia alitaka vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe vifutiliwe mbali.Siku ya Jumatatu azimio lililoafikiwa katika kikao hicho lilikashifiwa na wengi kuwa halikuchambua kwa undani tatizo la njaa duniani.
No comments:
Post a Comment