KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Kenya yaanza msako msitu wa Mau


Maafisa wameanza kufanya msako katika msitu wa Mau nchini Kenya, kuwaondoa watu waliosalia tangu kumalizika kwa muda uliopangwa na serikali kuwataka waondoke.
Mito mingi ya Kenya, vyanzo muhimu vya maji, imekauka na serikali inataka kurejesha uhai wa vyanzo hivyo.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, idadi kubwa watu kati ya familia 20,000, tayari wameshaondoka katika mashamba yao kwenye msitu huo.



Lakini mwandishi wa BBC katika eneo hilo anaeleza kuwa wengi wao hawana kwa kwenda na sasa wanaishi katika mazingira duni kando ya mipaka ya msitu wa Mau.

Kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita, zaidi ya hekari 100,000, robo ya msitu huo wa hifadhi - ilifyekwa na watu kuhamia kuendeleza maisha yao.

No comments:

Post a Comment