KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Japan wakwerwa na tarumbeta


Motoaki Inukai, rais wa Chama cha Soka cha Japan (JFA) ametaka ushangiliaji wa matarumbeta,Vuvuzela upigwe marufuku wakati wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
Fifa awali ilikataa wito wa kupiga marufuku matarumbeta hayo yaliyotengenezwa kwa plastiki.

Japan sasa imewataka maafisa wa Afrika Kusini kupiga marufuku Vuvuzela, baada ya mchezo wa kirafiki na wenyeji hao wa Kombe la Dunia mwishoni mwa wiki.

Inukkai amesema matarumbeta hayo yakihanikiza mtu hawezi kujisikia anachosema mwenyewe. Ameongeza atalipeleka suala hilo kwa rais wa Fifa Sepp Blatter. Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa Port Elizabeth, Afrika Kusini na Japan hazikufungana.

Mlinzi wa Japan Tulio amesema wakati zikivurumishwa tarumbeta hizo "huwezi hata kuwasikia wachezaji wenzako wanasema nini kutoka umbali wa mita mbili tu."

No comments:

Post a Comment