KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Gerrard yu tayari kuikabili Man City


Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard anamatumaini atakuwa amepona kuikabili Manchester City siku ya Jumamosi baada ya kusumbuliwa na nyonga.
Wakati wa mchezo na Birmingham tarehe 9 Novemba, Gerrard aliigia akiwa mchezaji wa akiba, lakini aliachwa katika timu ya taifa ya England iliyocheza na Brazil baada ya kuonekana hajaimarika.

Amesema baada ya mchezo na Birmingham alikuwa anajisikia mchovu sana.

Lakini kwa sasa amesema anajisikia vizuri zaidi. Lengo ni kupata mazoezi mazuri kwa wiki nzima hivyo atakuwa kwa mchezo na Man City.

Gerrard amekiri hakuwa tayari kurejea uwanjani dhidi ya Birmingham katika mchezo wake wa kwanza tangu alipoumia wakati England ilipocheza na Ukraine tarehe 10 mwezi Oktoba.

No comments:

Post a Comment