KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, November 17, 2009
HIJJA
HIJJA
HIJJA NI NGUZO KATIKA NGUZO ZA UISLAMU.
IBAADA YA HIJJA INA UMUHIMU WENYE MFUMO WA ULAZIMA WAKUITEKELEZA JUU YA KILA MTU AMBAE NI MUISLAMU.
IBAADA YA HIJJA INAFANYIKA KATIKA NCHI TAKATIFU YA SAUDIA ARABIA.
WAISLAMU TUNACHUKULIA NCHI YA SAUDIA KAMA CHIMBUKO LA HAKI KWA DUNIA NZIMA KUPITIA MUONGOZO WA NABII IBRAHIMU, ISMAIL NA MUHAMMAD (S.A.W).
NABII IBRAHIMU ALIZALIWA KATIKA ARDHI YA IRAQ, LAKINI KATIKA MAPITO YAKE, ALIWEZA KUMUOA MWANAMKE(SARAH) KUTOKA KATIKA BARA LA ASIA NA MWINGINE (HAJIRI) KUTOKA KATIKA BARA LA AFRIKA. NABII IBRAHIMU ALIKUWA NA WANAWAKE WA WILI AMBAO NI SARAH KAMA MKE WA KWANZA NA HAJIRI KAMA MKE WA PILI.
WANAWAKE HAO WALIWEZA KUPATA WATOTO (ISMAIL KAMA MTOTO WA KWANZA NA ISAKA KAMA MTOTO WA PILI).
KIZAZI CHA ISMAIL NDIO UZAO WA WARABU NA KIZAZI CHA ISAKA NDICHO KIZAZI CHA WAISRAEL.
WARABU NA WAYAHUDI CHIMBUKO LAO NI MOJA NA NI WATOTO WA BABA MMOJA NA MAMA TOFAUTI KUTOKA KATIKA MABARA(ASIA, SARAH NA AFRIKA, HAJIR) TOFAUTI NA RANGI TOFAUTI(ASIA MWEUPE NA AFRIKA MWEUSI)
MTAZAMO WA MGAWANYO WA MTOTO NA MUONGOZO
KUTOKANA NA KUWA MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA NA NI MWENYE UJUZI WA HALI YA JUU. MUNGU ALIMPA NABII IBRAHIMU MKE WA KWANZA AKIWA NI SARAH. UKINGALIA WATU HAO WALIKAA MUDA MREFU BILA KUPATA MTOTO MPAKA KUFIKIA UZEE. JAMBO LAKUSHANGAZA MWENYEZI MUNGU ALIMPITISHA HAJIRI KATIKA AMRI YA SARAH, AKAMSHAWISHI(SARAH) MME WAKE(NABII IBRAHIMU) KUMUOA (HAJIRI) KWA LENGO LA KUPATA MTOTO.
KITENDO HICHO CHA SARAH, KUMRIDHIA MME WAKE KUMUOA HAJIRI KAMA MKE WAPILI, KWELI KILIZAA MATUNDA. NABII IBRAHIMU ALIMCHUKUWA HAJIRI KUTOKA MIKONONI (ALIKUWA NI KIJAKAZI NA MILIKI YA SARAH) MWA SARAH NA WAKAPATA MTOTO WAO WA KWANZA AMBAE NI NABII ISMAIL.
FUNZO:
MUNGU ANAPOTAKA KUONESHA UWEZO WAKE HANA HARAKA, KWASABABU KILA JAMBO TAYARI AMEISHA LIPANGA. BAADA YA NABII IBRAHIMU KUMPATA MTOTO WA KWANZA AMBAE NI ISMAIL, MUNGU ALIMUAMURU KUHAMA NCHI NA KUWAPELEKA MWANAE ISMAIL NA MKE WAKE(HAJIR) KATIKA NCHI TAKATIFU YA SAUDIA ARABIA.
BAADA YA NABII IBRAHI KUFIKA NAO KATIKA ARDHI YA SAUDIA, KULIKUWA HAKUNA MAJI AU MMEA WOWOTE KATIKA JANGWA. LAKINI KUTOKANA NA DUA YA NABIII IBRAHIM JUU YA MKE WAKE NA MWANAE, ALIWAACHA KATIA MIKONO YA MUUMBA KISHA AKAONDOKA.
KILICHOFUATA MAMA WA ISMAIL (HAJIR) ALIHANGAIKA NA KUTEMBEA ZAIDI YA KILOMITA SITA (SAFA NA M.) AKIMTAFUTIA MWANAE MAJI, LAKINI MWENYEZI MUNGU ALITOA MAJI YA ZAMZAM KUTOKA CHINI YA MIGUU (ARDHINI ALIPOKUWA AKISIRIBA AU AKISAZA MIGUU)YA ISMAIL. KISIMA HICHO CHA MAJI YA ZAMZAM KINAJULIKANA KWA UBORA WA MAJI NA MAJISAFI WALA DUNIANI HAKUNA MFANO WAKE.
MAJI YA ZAMZAM HAYACHAFUKI WALA HAYAKAUKI, HATA KAMA YATACHOTWA NA WATU ZAIDI YA MILIONI AU BILIONI.
BAADA YA HAPO MUNGU ALIMPA AMRI NABII IBRAHI YA KUMCHINJA MWANAE WA PEKEE(ISMAIL). LAKINI MUNGU ALIMKOMBOA NA KIFO BAADA YA KUONA KWAMBA NABII IBRAHIMU YUKO TAYARI KUTEKELEZA AMRI YA KUMCHINJA MWANAE ISMAIL.
UMUHIMU MKUBWA WA IBAADA YA HIJA UNACHUKUWA NAFASI KUMBWA YA MAPITO YA NABII IBRAHIM, HAJIRI NA ISMAIL. NABII IBRAHI ALIPEWA RAMANI NA MUNGU YA KUMPELEKA MKEWE HAJIRI (MWANAMKE MUAFRIKA) NA MWANAE ISMAIL KATIKA NCHI TAKATIFU YA SAUDIA ARABIA. KATIKA NCHI HIYO NDIPO TUNAPOKUTA KIBLA YA KIISLAMU (KAABA) HAPA KWENYE KAABA NDIPO KATIKATI YA DUNIA. UKIPIMA KIPIMO CHOCHOTE KWA UPANDE WA MASHARIKI MAGHARIBI, UTAPATA SENTA YAKE KATIKA KAABA.
KWA KIFUPI KAABA NI DIRA YA WATU WANAOTEMBELEA SAYARI (MWEZI….N.K) KAMA WANA SAYANSI, WANATAMBUA NYUMBA HIYO KWAJINA LA BLACK STONE.
HAPA KUNA JIWE LILILOSHUSHWA NA MALAIKA GABLIERI KUTOKA MBINGUNI. JIWE HILI LILIKUWA KAMA RAMANI YA SEHEMU AMBAKO NYUMBA YA IBAADA YA MUNGU INATAKIWA KUJENGWA.
KAABA NI JENGO AMBALO LIMEJENGWA KWA UTAALAMU WA HALI YA JUU NA UBORA WA HALI YA JUU. UKIANGALIA RAMANI YA KAABA UTAONA KWAMBA SIO UJENZI WA KUBAHATISHA. KWASABABU KILA KONA YA KAABA INAMASHARIKI YAKE.
NA HISABU ZAKE ZIPO KATIKA MFUMO WA KITAALAMU ZAIDI. JENGO LA KAABA LILIJENGWA NA BABA YETU ADAMU NA KISHA BAADAE LILIKUJA KUBORESHWA NA NABII IBRAHIMU NA MWANAE ISMAIL. UKIFIKA KARIBU NA KAABA (MAKAMU IBRAHIMU) UTAKUTA KUNA ALAMA YA NYAYO ZA MIGUU YA NABII IBRAHIMU, KAMA USHAHIDI WA VIZAZI VYA BAADAE. KWA BAADAE NABII MUHAMMAD (S.A.W) ALIKUJA KUKOMBOA JENGO LA KAABA PINDI LILIPOKUWA LIMEVAMIWA NA WATU WASHIRIKINA. WASHIRIKINA HAO WALIKUWA WAMEFANYA NYUMBA HIYO YA KAABA KAMA HIFADHI YA MIUNGU YAO MIA TATU SITINI (360 gods).
BAADA YA NABII MUHAMMAD KUIKOMBOA MAKKA, KWA SASA IBAADA YA HIJJA INAENDELEA KAMA KAWAIDA.
NABII MUHAMMAD (S.A.W) ANATOKANA NA KIZAZI CHA ISMAIL MWANA WA BABA YETU WA IMANI NABII IBRAHIMU.
KIZAZI CHA ISRAEL ( ISAKA) KILIPOKEA VITABU(TORATI, ZABURI NA INJIRI) VITATU VYENYE MUONGOZO NA MITUME (ISAKA, YAKOBO, MUSA, HARUNA, YOSHUA, SAMWELI, DAUDI, SULEIMANI, YOHANA, YESU……..LAKINI MIOYO BAADHI YA WAYAHUDI WALISHINDWA KUKUBALI NA KULINDA AMRI NA SHERIA ZA MUNGU NA MARANYINGINE WAKAWAUA MANABII WALIOTUMWA KWAO.
WENGI SANA LAKINI KIZAZI CHA WARABU (ISMAIL) KILIPOKEA KITAMBU CHA MWISHO CHENYE UJUMBE WENYE MFUMO WA MKUSANYIKO WA VITABU VYOTE VILIVYOPITA KATIKA KIZAZI CHA WANA
WA ISRAEL.
UTEKELEZAJI WA IBAADA YA HIJJA UNAFANYWA KATIKA NJIA KUU MBILI.
NIA
UTENDAJI
NIA:
NIA NI MFUMO WA MARIDHIANO BAINA YA MWILI NA NAFSI.
NAFSI NI MUUNGANO BAINA YA ROHO NA MWILI. BINAADAMU HAWEZI KUTENDA JAMBO FULANI BILA IDHINI YA NAFSI YAKE NA ATAKAPOLIFANYA JAMBO HUSIKA, BASI ATAJIKUTA KATIKA UTENDAJI WA KUJILAZIMISHA KUFANYA JAMBO HUSIKA. IKIWA MTU ATAPENDA JAMBO (KULA, KUNYWA, KUTEMBEA, KUSOMA…..N.K) FULANI, ATAJIKUTA AKILITENDA KATIKA MFUMO WA UPENDO NA FURAHA. UPENDO NA FURAHA NDIO MSINGI WA AMANI NA UTULIVU NDANI YA NAFSI YA MTU. UTULIVU WA KAZI UNATOKANA NA NIA YA NAFSI.
UTENDAJI:
SIKU ZOTE UTENDAJI UNATOKANA NA MARIDHINO YA FIKIRA BAINA YA ROHO NA MWILI. MWILI HAUWEZI KUTENDA AU ROHO KUTENDA JAMBO FULANI BILA KUWA NA USHIRIKIANO.
KILA TENDO HUONGOZWA NA MTAZAMO WA NAFSI HUSIKA.
SIKU ZOTE UTENDAJI UNAENDANA NA GHARAMA. UNAPOSAFIRI UNAHITAJI NAULI, PESA YA ULINZI WA NAFSI YAKO NA MARANYINGINE KUWASAIDIA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, KUTOKANA NA MALI AU PESA YAKO.
UNAPOKUJA KWENYE IBAADA YA HIJJA UTAONA KWAMBA NILAZIMA KWA KILA MUISLAMU KUITEKELEZA.
LICHA YAKUWA IBAADA YA HIJJA IMELAZIMISHWA KWA WAISLAMU, MWENYEZI MUNGU AKATOA OFA KWA MASIKINI. KWA MAANA HII MUISLAMU MWENYE UWEZO WA KINAFSI NA KIFEDHA NDIE MWENYE NAFASI YA ULAZIMA WA KUTEKELEZA IBAADA HIYO KWA MATENDO.
KWA MUISLAMU MASIKINI, YEYE ANAWEZA KUTEKELEZA IBAADA YA HIJJA KWA NIA. KWASABABU NIA YA KWENDA KUFANYA IBAADA YA HIJJA IPO NDANI YA NAFSI YAKE LAKINI KWA MATENDO TAYARI HUJIKUTA KATIKA HALI NGUMU YA UCHUMI.
IBAADHA YA HIJA INACHUKUWA NAFASI YA TANO AMBAYO NIYA MWISHO KATIKA NGUZO ZA KIISLAMU.
IBAADA YA HIJJA KAMA NGUZO YA KIISLAMU INAKUJA BAADA YA NGUZO HIZI:
1. KUTOA SHAHADA (KUAMINI KWAMBA MWENYEZI MUNGU NI MMOJA NA KUAMINI KWAMBA NABII MUHAMMAD (S.A.W) NI MJUMBE WAKE)
2. KUSIMAMISHA SALA (NIWAJIBU KWA KILA MUISLAMU KUSIMAMISHA SALA TANO KWA SIKU)
3. KUTOA ZAKA (ZAKA NIFUNGU FULANI LINALOTOKANA NA MALI YA MATAJIRI KUELEKEA WATU MASIKINI)
4. KUFUNGA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI (MWEZI WA RAMADHANI NI MWEZI WENYE UMUHIMU NA NDIO MWEZI ULIOSHUSHWA NDANI YAKE KITABU KITUKUFU CHA QURAN)
5. KWENDA MAKKA KWA MWENYE UWEZO( MWENYEZI MUNGU AMETUMIA NJIA YA KUONESHA WAISLAMU KWAMBA UISLAMU NI MWEPESI NA NIRAHISI. IKIWA UNA UWEZO WA KIAFIA NA FEDHA UNATAKIWA KUTEKELEZA IBAADA YA HIJJA NA IKIWA UNAUPUNGUFU WA FEDHA AU KINGUVU LAKINI UNA NIA MWENYEZI MUNGU ANAKUANDIKIA THAWABU KAMA YULE MTEKELEZAJI WA SAFARI YA MATENDO).
WAISLAMU TUNAJIFUNZA MAMBO MENGI KATIKA UTEKELEZAJI WA IBAADA HII YA HIJJA.
KUNA :
1. KUTEMBELEA PAHALA ALIPOSIMAMA NABII IBRAHIMU (BABA YETU WA IMANI) AKAWEZA KUMUOMBA MUNGU WAKE.
2. KUMBUKUMBU YA SAFARI YA IBRAHIMU, HAJIRI NA MWANAE ISMAIL KATIKA ARDHI TAKATIFU YA MAKKA.
3. SAFARI NGUMU YA MAPITO YA HAJIRI KATIKA KUSAKA MAJI YA MWANAE ISMAIL JANGWANI. ILICHUKUWA TAKIRIBANI KILOMITA SABA (KM 7 KATIKA SAFA NA M.)
4. ISMAIL KUWA CHANZO CHA MAJI MATUKUFU NA MASAFI KULIKO MAJI YOTE DUNIANI AMBAYO NI MAJI YA ZAMZAM.
5. JENGO LA KAABA LILILOJENGWA NA NABII IBRAHIMU NA MWANAE ISMAIL.
6. NYAYO AU ALAMA ZA MIGUU YA NABII IBRAHI ALIPOKANYAGA, PALIBAKI KAMA USHAHIDI NA KUMBUKUMBU KWA VIZAZI VIJAVYO.
7. KUSHUHUDIA ALIPOZALIWA NABII MUHAMMAD NA ALIPOZIKWA PAMOJA NA MASWAHABA WAKE.
8. KUFUTIWA MADHAMBI YOTE NA KUTAKASIKA KAMA MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA HANA DHAMBI
9. ……………………………….N.K.
KWA KWELI IBAADA YA HIJJA NI IBAADA AMBAYO INATEKELEZWA NA WACHA MUNGU WALA HAKUNA KUBAHATISHA KATIKA IBAADA YA HIJJA.
KUNA WATU WENGI AMBAO NI WAISLAMU WANA UWEZO WA NGUVU YA MWILI NA ROHO (NAFSI) FEDHA AU MALI YA KUWAWEZESHA KUTEKELEZA IBAADA YA HIJJA LAKINI BADALA YA KUTEKELEZA IBAADA HUSIKA HUJIKUTA KATIKA SAFARI ZA KUONGEZA MALI NA PESA KATIKA NCHI ZA MAGHARIBI, AFRIKA, MAREKANI…….N.K, BILA KUJALI IBAADA YA HIJJA.
KUNA BAADHI YA WAISLAMU WENYE GHOFU YA KWENDA MAKKA KATIKA UJANA WAO KUTOKANA NA UTAMU WA STAREHE ZAO ZA HAPA DUNIANI. KWA MAANA HII WANASUBIRI KWANZA WAKARIBIE UZEE KISHA WAENDE KUTEKELEZA IBAADA YA HAJJI KATIKA MFUMO WA KUOKOKA.
HALI HII NI YENYE MFUMO HATARI SANA KWASABABU HAKUNA MTU MWENYE KUJUA NIWAKATIGANI ATAFARIKI.
MUISLAMU HARUHUSIWI KUTUMIA HELA YA DHULMA AU YA BIASHARA HARAMU KATIKA IBAADA YA HIJJA. KUNA BAADHI YA WAISLAMU WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA YA KIPATO CHA DHULMA AU BIASHARA HARAMU, WATU HAO HAWARUHUSIWI KUTOA ZAKA AU KUTUMIA PESA HIYO KWENYE IBAADA YA HIJJA.
UKWELI WA MAMBO:
SI KUSEMA KWAMBA WAISLAMU WENGI MATAJIRI HAWANA HAJA YA KWENDA HIJJA LA! BALI WENGINE HUWA NA MALI ZA HARAMU KWAMAANA HIYO WANAKUWA WAKIGHOFIA KUITUMIA KATIKA IBAADA YA ZAKA NA HIJJA.
USHIRIKIANO
USHIRIKIANO KATIKA IBAADA YA HIJJA NI MKUBWA BAINA YA WAISLAMU NA WALE AMBAO SIO WAISLAMU. WAISLAM WANAPOJIANDAA KWENDA KUFANYA IBAADA YA HIJJA WANATAKIWA KUJIANDAA KIMWILI NA KIROHO. NDIO MAANA KATIKA UWANJA WA IBAADA YA HIJJA UTAWAKUTA WATU WA AINA MBALIMBALI(WAZUNGU, WARABU, WAAFRIKA, WACHINA, WAJAPANI…………MABARA YOTE YAKO PALE SAUDIA ARABIA).
KATIKA IBAADA YA HIJJA UTAKUTA KILA AINA YA KABILA (WAZARAMU, WAKULIA, WALUO, WAGANA, WAGANDA, WANYAMLENGE, MAIMAI, WAHUTU, WATUSI, WATWA, WASOMALI, WAKWERE, WANUBI, WAZURU,………………………………..N.K).
KATIKA IBAADA YA HIJJA KUNA CHEO KIMOJA NACHO NI UCHAMUNGU. KILA MTU MWENYE KUSHIRIKI KATIKA IBAADA YA HIJJA ANATAKIWA KUACHA CHEO (URAISI, UMENEJA, UKURUGENZI, UPOROFESA, UDAKITARI, UKUPWA WA KIJESHI AU WAKIFALME, UBABA, UMAMA, UJOMBA,………N.K)CHAKE NYUMBANI KWAKE SIO MBELE YA HIMAYA YA MUNGU.
UNAPOKUWA KATIKA UWANJA WA HIJJA UTASHUHUDIA MAMBO MENGI NAYENYE KUFURAHISHA MAISHANI MWETU. KAMA MTU FULANI ATAJIKWAA NA KUMKANYAGA MFALME AU RAISI, UNAWEZA KUSHANGAA MTOAJI WA KWANZA WA SAMAHANI NI RAISI AU MFALME.
MAVAZI YA HIJJA:
MAVAZI YA HIJJA YAKO AINA MBILI. KUNA MAVAZI YA KIUME NA MAVAZI YA KIKE. WANAUME WANATAMBULIKA KWA MAVAZI YAO NA WANAWAKE KWA MAVAZI YAO. KUNA BAADHI YA SEHEMU AMBAZO WANAWAKE WANACHANGANYIKA NA WANAUME KATIKA IBAADA YA HIJJA.
KUNYOA:
KUNA WAKATIFULANI AMBAO MAHUJAJI WANATAKIWA KUNYOA NA MARANYINGINE KUNA KIPINDI MAHUJAJI HAWARUHUSIWI KUWINDA AU KUFANYA BIASHARA YOYOTE. KATIKA ENEO LA IBAADA YA HIJJA , KUNA UTARATIBU WAKE WA KIIBAADA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Good
ReplyDelete