KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Muswada wa katiba mpya nchini Kenya unawasilishwa hii leo


Kenya kujadili katiba mpya

Muswada wa katiba mpya nchini Kenya unawasilishwa hii leo, kwa ajili ya kujadiliwa na wananchi kwa siku 30.
Muswada huo unapendekeza mamlaka ya rais wa nchi yapunguzwe, na waziri mkuu kupewa nguvu zaidi.

Mapendekezo mengine ni kuondolewa kwa utawala wa majimbo na kuanzisha mikoa zaidi.

Hata hivyo baada ya ghasia za uchaguzi mwaka jana, kuna wasiwasi kuwa hatua hizi zitazidisha migawanyiko ya kikabila.

Muswada wa awali wa katiba ulikataliwa na wakenya katika kura ya maoni iliyofanyika Novemba 2005.

No comments:

Post a Comment