KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 18, 2009

Afrika yataka fidia ya uchafuzi wa mazingira

Viongozi wa Africa wanaokutana Ethiopia wanasema wamekubaliana kiasi cha fedha wanachitaka kufidiwa kwa athari za mabadiliko ya hewa duniani.
Hata hivyo, wamesema watafanya kiasi hicho siri mpaka mkutano wa kimataifa wa mazingira Denmark mwezi Disemba.

Tangazo hilo limetolewa wakati jopo la mataifa 10 ya Afrika lilipokutana Addis Ababa kukamilisha msimamo wao.

Kiongozi wa Ethiopia alisema Afrika inastahili kulipwa fidia kwa athari zilizosababishwa na mataifa tajiri kwa uchafuzi wa hewa.














Mwandishi wa BBC aliyeko Addis Ababa, anasema kiasi hicho kinatarajiwa kuwa mabilioni ya dola kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment