KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 18, 2009

Misri na Algeria zazidi kutupiana maneno


kuu wa shirikisho la soka la Algeria amemlaumu mwenzake wa Misri kwa ghasia zilizotokea Jumamosi wakati nchi hizo zilipokutana Cairo kuwania nafasi ya kucheza kombe la dunia.
Watu wasiopungua 32 walijeruhiwa baada ya mechi hiyo, na baada ya hapo biashara kadhaa zenye uhusiano na Misri zilivamiwa mjini Algiers.

Misri imeongeza malalamiko yake kuhusu mashambulio hayo. Baada ya ushindi wa magoli mawili kwa sifuri, kundi la timu hizo halijapata mshindi - Misri na Algeria zinakutana Khartoum kuamua mshindi.

Maafisa wa polisi 15,000 wa Sudan watakuwa kazini wakati wa mechi hiyo kuzuia uwezekano wa kutokea ghasia.

Mashabiki wa pande hizo mbili watatenganishwa kikamilifu ndani ya uwanja. Kila nchi itapata tiketi 9,000, katika uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 35,000.

No comments:

Post a Comment