KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 2, 2009

Mabaki yadhaniwa ya ndege iliyotowek!

Bado haijathibitishwa mabaki hayo ni ya ndege iliyotoweka ya Air France.
Ndege za kijeshi za Brazil zinazoitafuta ndege ya Air France iliyotoweka ikiwa na abiria 228 kwenye bahari ya Atlantic, wamefanikiwa kuona baadhi ya mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege.



Ndege za kijeshi za Brazil zinazoitafuta ndege ya Air France iliyotoweka ikiwa na abiria 228 kwenye bahari ya Atlantic, wamefanikiwa kuona baadhi ya mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege.
Baadhi ya vitu vya kwanza kabisa kuonekana ni mafuta yaliyomwagika, kiti cha abiria na vinginevyo, vilivyokutwa yapata kilometa 650 kaskazini-mashariki mwa kisiwa cha Fernando de Noronha kinachomilikiwa na Brazil, taarifa hizo ni kwa mujibu wa jeshi la anga la Brazil.

Kazi ya kutafuta ndege hiyo bado inaendelea, lakini uthibitisho utapatikana tu mara baada ya kuviopoa na kuvitambua vitu hivyo. Swala hilo litachukua muda kwasababu kutokana na umbali, boti ya kwanza inaelezwa kuwa itafika eneo hilo Jumatano.

Uhakika
Maafisa wanasema, watahitaji kujiridhisha kwa kulinganisha baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya ndege kuwa kweli mabaki hayo yametoka kwenye ndege iliyotoweka.

Msemaji wa jeshi la anga la Brazil, Kanali Jorge Amaral, ameeleza kuwa mabaki hayo yanayodhaniwa kuwa ya ndege yalionekana kutoka angani wakati ndege zinazofanya shughuli ya utafutaji zilipopita eneo hilo mapema Jumanne.

"Yapata saa kumi na moja na nusu majira ya Brazil, wataalam katika ndege ya kijeshi aina ya C-130 walifanikiwa kuona mabaki hayo katika sehemu mbili tofauti zikiwa umbali wa kilometa 60 kutoka kila moja", alieleza Kanali Amaral.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Herve Morin amesisitiza kuwa bado hakuna ushahidi wowote kuweza kueleza kitu kilichosababisha kupotea kwa ndege hiyo.

Utafutaji
Ndege za uokoaji za Brazil, Ufaransa na nchi nyingine zimeelekeza nguvu zao kutafuta mabaki katika eneo ambalo ni katikati ya umbali kwenda Brazil au Afrika Magharibi, wakitumai kupata mawasiliano na vifaa vilivyo ndani ya ndege hiyo aina ya Airbus 330 - 200.

Ndege hiyo yenye safari namba AF 447 ilikuwa ikisafiri kutoka Brazil ikielekea Ufaransa ikiwa imebeba watu 228.

Abiria hao walikuwa raia wa mataifa mbalimbali. Wafaransa 61, Wabrazili 58, Wajerumani 26 na wengine walikuwa kutoka nchi za Uswisi, Uingereza, Lebanon, Hungary, Ireland, Norway na Slovakia.

No comments:

Post a Comment