KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 2, 2009

Somalia "hali mbaya" - Oxfam




Mratibu wa shirika la misaada la Oxfam amesema hali ya kibinaadam ni "mbaya sana" nchini Somalia, kuwahi kuonekana barani Afrika kwa miaka mingi.
Wengi wa maelfu ya wananchi wa Somalia waliokimbia makazi yao, wanaishi kwa chakula kidogo na wengine hawana hata mahala pa kujihifadhi amesema mratibu huyo, Hassan Noor.

milio ya risasi

Wakazi wa Mogadishu wamekuwa wakikimbia mapigano makali kati ya makundi ya wapiganaji wanaopambana na majeshi yanayoungwa mkono na serikali.

Watu wanaendelea kukimbia mji mkuu huo, huku milio ya risasi ikisikika.

Mwandishi wa BBC Mohamad Olad Hassan akiwa Mogadishu anasema wakazi wa mji huo wametumia mwanya wa kutulia kwa muda kwa mapigano, kuukimbia mji huo, huku wakiwa wamebeba mizigo midogo midogo.

maji kidogo

Maelfu ya watu wanaokimbia makazi yao, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wamekimbilia Afgooye, kusini mwa mji huo, ambapo wanajihifadhi chini ya miti huku kukiwa na chakula na maji kidogo ya kunywa.

Hassan Noor ameiambia BBC kuwa hali katika mji wa Mogadishu ni "mbaya mno".

"Hali inasikitisha sana", amesema mratibu huyo.

kuhara

Ameongeza kusema, "Kuna mamia ya watoto wakiwa na mirija ya kitabibu mikononi mwao. Wengine wamepoteza fahamu kabisa, wakiugua kila aina ya magonjwa, hasa kuhara na kipindupindu."

Bw Noor amesema "Nimeona hali ilivyo Darfur, Kaskazini mwa Uganda, baadhi ya maeneo ya Kongo, lakini kinachotokea sasa hivi Somalia, ni hali mbaya ya kibinaadam kuwahi kuonekana Afrika kwa miaka mingi."

Makundi ya wanamgambo ya Hisbul-Islam na al-Shabab yamekuwa yakipambana vikali na wanajeshi wanaoungwa mkono na serikali tangu Mei 7, na kusababisha zaidi ya raia elfu 60 kukimbia makazi yao.

No comments:

Post a Comment