KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, June 1, 2009

MSIKITI WAVAMIWA MISAHAFU YACHANWA










MSIKITI WAVAMIWA MISAHAFU YACHANWA

KUNDI LA VIJAA WA KIHUNI LIMEVAMIA NA KUVUNJA MLANGO WA MASJID MASHA, MAARUFU KWA JINA LA MSIKITI
WA WARANGI, ULIOPO MBEZI MWISHO, BARABARA YA MOROGORO JIJINI DAR ES SALAAM. BAADA YA KUFANYA UVAMIZI HUO, WALICHANA MISAHAFU, NA KUMWAGA DAMU NDANI YA MSIKITI NA BAADA YA HAPO WAKAIBA KIFAA CHA KUKUZIA SAUTI ( AMPLIFIER ) NA KUTOWEKA.TUKIO HILO LIMEARIFIWA KUTOKEA HIVI KARIBUNI MCHANA KABLA YA SWALA YA ADHUHURI NA KURIPOTIWA KITUO CHA POLISI.

AMIRI WA BARAZA KUU WILAYA YA KINONDONI USTADH ABUBAKARI AHMED ABDUL SWAMAD , AMBAYE ALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHUHUDIA UHALIFU HUO, ALISEMA KABLA YA KUTOKEA UHALIFU HUO, BWANA MMOJA ANAYE TAMBULIKA KWA JINA LA SIDE , AMBAYE ANAISHI JIRANI NA MSIKITI HUO, SIKU ZA KARIBUNI ALIFIKA MSIKITINI HAPO NA KUWAAMBIA WAUMINI WALIOKUWA WAKITOKA KATIKA SWALA KWAMBA ANAKERWA SANA NA ADHANA ZA ALFAJIRI , NA AKAWATAKA KUACHA KUTOA ADHANA HIYO KWANI INAMSABABISHA KUKOSA USINGIZI.

BAADA YA TUKIO HILO, BWANA SIDE HAJULIKANI ALIPOKIMBILIA NA POLISI WANAFUATILIA KWA KARIBU CHANZO CHA UHALIFU HUSIKA.


QURANI :

WENYEZI MUNGU ANASEA “ NA KWA ( AJILI YA KULETA ) HAKI ( ULIMWENGUNI NDIO ) TUMETEREMSHA ( QURAN ) . NA HATUKUKULETA ( NABII MUHAMMAD ( S.A.W ) ) ILA UWE MTOAJI WA KHABARI NJEMA NA MWONYAJI.

( 17 : 105 )

NA MTIINI MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE WALA MSIZOZANE ( MSIGOMBANE ), MSIJE MKAHARIBIKIWA NA KUPOTEA NGUVU ZENU, NA MVUMILIENI ( MSTAHAMILIANE ). BILA SHAKA MUNGU YU PAOJA NA WANAOVUMILIA.

( 8 : 46 )

NA JISAIDIENI ( KATIKA MAMBO YENU ) KWA KUSUBIRI NA KWA KUSALI , NA KWAHAKIKA JAMBO HILONIGUMU USIPOKUA KWA WANYENYEKEVU.

( 2 : 45 )

AMBAO WANA YAKINI YA KWAMBA WATAKUTANA NA MOLA WAO NA YA KWAMBA WATAREJEA KWAKE.

( 2 : 46 )


BIBLIA

YESU “ BASI JIANGALIENI , MIOYO YENUISIJE IKAELEMEWA NA ULAFI, NA ULEVI, NA MASUMBUFU YA MAISHA HAYA;
SIKU ILE ( KIYAMA ) IKAWAJIA GHAFLA , KAA MTEGO UNASAVYO; KWA KUWA NDIVYO ITAKAVYO WAJILIA WATU WOTE WAKAAO JUU YA USO WA DUNIA NZIMA.BASI KESHENI NINYI KILA WAKATI , KIOBA , ILI PATE KUOKOKA KATIKA HAYO YOTE YATAKAYO TOKEA, NA KUSIMAMA MBELE ZA MWANA WA ADAMU.

( Luka 21 : 34…38 )

No comments:

Post a Comment