KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, May 1, 2009

kumchinja mnyama








KUMCHINJA MNYAMA LAZIMA UTAJE KINA LA MUNGU
KUTOKA NDANI YA BIBLIA NA QURAN

KILA JAMBO MAISHANI, LINA MWONGOZO WAKE. MWONGOZO WA KILAJAMBO UNATOKANA NA MTENGENEZAJI. KIWANDA CHA SIMU YA NOKIA, KINATENGENEZA SIMU ZA NOKIA NA KUMPA MTUMIAJI MUONGOZO WA MATUMIZI YAKE (SIMU). HUWEZI KUTUMIA VOCHA YA TIGO UKIWA NA LAINI YA ZANTEL AU VODACOM.UNACHO HITAJI KUKIFANYA, NI KUTUMIA VOCHA AMBAYO INAINGILIANA NA LAINI YAKO, KINYUME CHAKE HUNA MAWASILIANO.

*MWENYEZI MUNGU ALIUMBA KILA KITU KATIKA ARDHI NA MBINGUNI, KWA MAPENZI YAKE NA KILA KIUMBE CHAKE ANAKIJUA.
HAKUNA KIUMBE KINACHOONGEZEKA AU KUPUNGUA, BILA MAPENZI YA MWENYEZI MUNGU.

MWENYEZI MUNGU ALIUMBA KILA MNYAMA NA NDEGE NA AKAWEZA KUWATENGENEZEA MFUMO WA MAISHA. VILE VILE MWENYEZI MUNGU ALIMPA BINAADAMU UWEZO WA KUWATUMIA WANYAMA HAO KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI, MOJAWAPO NI KUWALA,KULIMA, ULINZI,USAFIRI, MAVAZI,MBOLEA, MAPAMBO,DAWA……….N.K.

KATIKA WANYAMA WANAOLIWA, MWENYEZI MUNGU AMETUHIMIZA KUWACHINJA KABLA HATUJAWAANDA KWA CHAKULA.

MTAZAMO WA KUCHINJA KATIKA VITABU VYA DINI ( MUOINGOZO WA MUNGU KWA WAJA WAKE ) TUMEELEZWA NA MUNGU, KUHUSU UTARATIBU WA MAANDALIZI YA WANYAMA WANAOLIWA.

EBU, TUANGALIE BAADHI YA AYA ZA VITABU KUHUSU KUCHINJA.



QURAN:
NA HAKUNA MNYAMA KATIKA ARDHI NA NDEGE ARUKAYE KWA MBAWA ZAKE MBILI, ILA NI UMATI KAMA NYINYI
(TUNADHIBITI KILA WALIFANYALO). HATUKUPUUZA KITABUNI
(MWETU) KITU CHOCHOTE. KISHA WATAKUSANYWA KWA MOLA WAO (AWALIPE).
(6: 38)
UKISOMA NA KUTAFAKARI AYA HII, UTAONA YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU HANA MFANO KATIKA UUMBAJI WAKE.

HATA KATIKA WANYAMA NA NDEGE , NI UMATI KAMA SISI BINAADAMU. WANYAMA WANAISHI KATIKA MAKUNDI KAMA SISI, WANYAMA WANAKULA KAMA SISI,WANYAMA WANAJISAIDIA KAMA SISI,WANYAMA WANA MAKAZI KAMA SISI, WANYAMA NA NDEGE WANAWEZA KUHAMA KUTOKA SEHEMU MOJA KWENDA SEHEMU NYINGINE NA MARANYINGINE KUVUKA MPAKA WA NCHI YAO NA KWENDA KATIKA NHI NYINGINE KUTAFUTA RIZIKI. WANYAMA NA NDEGE WANA MPANGILIO WA VIZAZI NA MALEZI KAMA BINAADAMU, WANYAMA HUA NA FURAHA NA HUZUNI KAMA SISI BINAADAMU, WANYAMA WANAHISI MAUMIVU KAMA SISI BINAADAMU, WANYAMA HUA NA BABA NA MAMA KAMA SISI BINAADAMU.WANYAMA WANA MDA WA KUFANYA KAZI NA MDA WAKUPUMZIKA KAMA SISIS BINAADAMU……………………………………………….N.K. KILA JAMBO LINALO FANYWA NA KILA KIUMBE HAPA DUNIANI, LINAANDIKWA NA MWISHO WAKE (KILA JAMBO ) NI KILA KIUMBE KITAPELEKA RIPOTI KWA MUUMBA WAKE. RIPOTI HIO INAHUSU MAISHA YA KILA KIUMBE,MATENDO,MANENO…………N.K. MWISHO WA KILA JAMBO NI KWAMWENYEZI MUNGU.



BIBLIA:

KWA MAANA KILA KIUMBE CHA MUNGU NI KIZURI, WALA HAKUNA CHA KUKATALIWA, KAMA KIKIPOKEWA KWA SHUKURANI , KWA KUWA KIMETAKASWA KWA NENO LA MUNGU NA KWA KUOMBA.
(1 TIMOTHEO 4 : 4,5)

KWA MUJIBU WA BIBLIA, KILA KIUMBE NI CHA MUNGU NA NIKIZURI.SASA IKIWA BINAADAMU ANAAMINI YA KWAMBA MUUMBA NI MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE, LAZIMA AKIONA VIUMBE ( WANYAMA, NDEGE, SAMAKI, MIMEA,MAJI, WATU………….N.K) WENGINE JUU YA ARDHI NA MBINGUNI, AWE ( BINAADAMU ) MWEPESI WA KUSHUKURU NEEMA ZA MWENYEZI MUNGU ZILIZOKO JUU YAKE. NA LAZIMA KILA JAMBO LITAKASWE KWA NENO LA MWENYEZI MUNGU. UKITAKA KUCHINJA MNYAMA AU NDEGE, KWA NZA TANGULIZA NENO LA MWENYEZI MUNGU, NI KAMA KUMPA TAARIFA YA KUSHUKURU KUHUSU KUPATA NYAMA HUSIKA NA KUOMBA MUNGU AIBARIKI NYAMA HIO. UNAPOCHINJA MNYAMA AU NDEGE , BILA KUTAJA NENO LA MWENYEZI MUNGU, NIKOSA NA NIDHAMBI KUBWA KABISA.UMEWEZA KUCHUKUA KIUMBE CHA MWENYEZI MUNGU KWA MABAVU, BILA OMBI WA LA SHUKURANI, KUMBUKA AHADI YA MWENYEZI MUNGU NI “ KILA KIUMBE KITARUDI KWANGU “
IKIWA WEWE NI MCHA MUNGU NA UNAOGOPA KUMUASI MUNGU BASI FUATA AMRI NA SHERI ZA YULE ALIEKUUMBA NA AKAUMBA KILA MAHITAJI YAKO KATIKA MFUMO WA HERI.


QURAN :

BASI KULENI KATIKA WALE WALIOSOMEWA JINA LA MWENYEZI MUNGU (WAKACHIJWA, SIO WALIOKUFA WENYEWE ).IKIWA NYINYI MNAZIAMINI AYA ZAKE.
(6 : 118 )

MWENYEZI MUNGU ANATUHIMIZA, KUTUMIA JINA LAKE KAMA UFUNGUO WA KUMWAGA DAMU YA MNYAMA AU NDEGE FULANI, ILI AWEZE (MWENYEZI MUNGU ) KUBARIKI NYAMA HUSIKA.

MWENYEZI MUNGU ANENDELEA KUTUHIMIZA, KUTOKULA WANYAMA AU NDEGE AMBAO WAMEKUFA WENYEWE. KATIKA AYA HII MNA MAZINGATIO KWA WATU WENYE AKILI. MNYAMA NAPOKUFA MWENYEWE HUWA NA ASILIMIA MIA MOJA YA MAGONJWA. KWA MFANO MNYAMA ANAPOKUFA MWENYEWE , DAMU HAITOKI MWILINI NA DAMU HUBEBA ASILIMIA MIA MOJA YA MARADHI YA MNYAMA HUSIKA.
IKIWA MNYAMA HUYO AMEKUFA KWA SABABU YA UGONJWA FULANI, VILE VILE UNAWEZA KUHAMIA AU KUHATARISHA AFYA ZA WALAJI.NDIO KAANA MWENYEZI MUNGU ANATUHIMIZA KUITOA
(DAMU) MWILINI MWA MNYAMA ANAYE CHINJWA. MWENYEZI MUNGU ANAMALIZIA AYA AKISEMA YAKWAMBA UJUMBE HUU UNAHUSU WALE WENYE KUMWAMINI MWENYEZI MUNGU.UKIASI AMRI YA MUNGU AKALA MNYAMA ASIECHINJWA KWA JINA LAKE, NA UKIJUA VIZURI NI KOSA NA UTAHUKUMIWA KWA KOSA LA KUASI AMRI YA KUCHINJA NA KULA KILICHO HALALI, HATA KAMA MNYAMA NI WAKO LAKINI KAUMBWA NA MUNGU.NA WEWE UMEUMBWA NA MUNGU, NA MWISHO WAKE UTAKUFA UTARUDI KWA MUNGU NA UTALIPWA KWA YALE ULIOKUWA UKIYATENDA.

BIBLIA :

BASI, MLAPO, AU MNYWAPO, AU MTENDAPO NENO LOLOTE, FANYENI YOTE KWA UTUKUFU WA MUNGU.
(1 WAKORINTHO 10: 31)

BIBLIA INATUELEZA KUHUSU UTUKUFU WA MWENYEZI MUNGU, YA KWAMBA MTANGULIZE MWENYEZI MUNGU KATIKA KILA JAMBO. UNAPOTEMBEA, KULA, KUNYWA, KUVAA, KATIKA SAFARI………..N.K.

QURAN

AMETUKUKA YULE AMBAYE MKONONI MWAKE UMO UFALME (WOTE); NAYE NI MWENYE UWEZA JUU YA KILA KITU.
(67: 1 )

AMBAYE AMEUMBA MAUTI NA UHAI ILI KUKUJARIBU (KUKUFANYIENI MTIHANI); NI NANI MIONGONI MWENU MWENYE VITENDO VIZURI ZAIDI. NAYE NI MWENYE NGUVU (NA) MWENYE MSAMAHA.
(67: 2)

No comments:

Post a Comment