KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, May 1, 2009

Kutana na Mungiki





Je unawajua Mungiki?
Kwa wenzetu wakenya mungiki ni kama kifo! ni jamii ya watu wafanyao uhalifu wa kufuru kwa wanajamii wenzao. Hawa ni zaidi ya majambazi! Kwani wana mfumo mzima wa uendeshaji unawahakikishia kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi! Serekari ya Raisi kibaki imejaribu kwa kila jinsi kupambana vikali na watu hawa na kati ya mapigano hayo maelfu ya raia wema wamepoteza maisha, makazi,mali zao na wengine wamepata ulemavu wa kudumu, wengine wamebakwa, wengine yatima na wajane na uharibifu mkubwa wa miundombinu. yaani jamaa wanaleta balaa la jehanamu kwa wananchi wa kenya!sasa tukiwa katika harakati za kujiunga na East Africa Community je tumefanya jitihada gani kulitafutia suluhisho hili swala la Mungiki? Maana kama tukiwa pamoja tutarithi mambo mengi pamoja na inawezekana kabisa kuwa na Mungiki wa Bongo na Uganda! Maana ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji! Sasa ni wakati mwafaka wa kutafuta suluhisho la jambo la kutisha na kuogopesha kama hili la Mungiki! Ukizingatia hao mungiki ni waafrika wenzetu unadhani ni jinsi gani waafrika twaweza kujikomboa? lini tutaweka kando fikra zetu pofu na potofu? Lini tutaweza kulinda kile tulichonacho kwa maslahi yetu sote? Lini tutaacha kuana kama wanyama poli? Lini tutakuwa waastaarabu na kukaa katika meza mmoja kama familia ya kiafrika na kujivunia amani na upendo na kulinda kila Mwenyezi Mungu alichotujalia? Kwa pamoja tutokomeza jamii mbovu kama za Mungiki na Mafisadi wa aina zote katika afrika yetu, lakini tukiacha ubinafsi na fitna twaweza fika mbali nasi tukawa wanamaendeleo wa dunia hii! na kubadilisha mfumo wa kuitwa dunia ya tatu tukawa dunia ya kwanza yenye furaha, upendo na amani
Mungu ibariki Afrika, Mungu wanusuru Wakenya toka kwenye Mikono ya Mungiki!

No comments:

Post a Comment