KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Sunday, May 17, 2009
Habari ya Papa Na Middle East
Pope risks more Israeli wrath as he calls for Palestinian state on visit to West Bank
Pope, Abbas discuss Mideast peace process
VATICAN CITY (AP) — Pope Benedict XVI discussed the Middle East peace process Saturday with Palestinian leader Mahmoud Abbas, who invited the pontiff to visit the Holy Land
Wiki hii imetawaliwa na Habari nyingi ila Habari ya papa kutembelea mashariki ya kati imekuwa nzito katika masikio ya watu duniani kote. Akiwa kiongozi mkubwa wa dini kutembelea maeneoya masharikiya kati wakati kama huu wa khali tete kati ya wapalestina,wayahudi na wairani, wote wakiwa katika vita ya maneno na kisera kuhusu swala la haki ya Uongozi wa mashariki ya kati.
Kauli yoyote kutoka kwa kiongozi huyu wa mmoja ya madhehebu yenye wafuasi wengi duniani na kati ya mmoja ya dhehebu lisilo na maelewano mazuri kiimani na dini ya kiyahudi inaweza kuchukuliwa kwa njia tofauti kabisa. Kauli yake yaweza kuwa kisu Kwa upande mmoja na kuwa faraja kwa upande mwingine.
Kwa kujua yote hayo vyombo vya Habari vya magharibi vilifuatilia kila hatua ya kiongozi huyo mkubwa tangu alipotua Jordan mpaka alipotua Israeli. Kwa umakini mkubwa aliongelea swala la mauaji ya kimbali yaliyofanywa kwa wayahudi na pia aliongelea uwepo wa taifa huru la Kipalestina! Kwa kufanya hivyo aliweza kuua ndege wawili kwa jiwe mmoja. Licha ya hivyo safari hii kwa kiasi haikuweza kutibu tofauti kati ya wapalestina na waisraeli pia haikuweza kutibu mahusiano kati ya wakatoliki na wayahudi kiimani. Je mtazamo wetu sisi waafrika ni upi! Nani yuko sawa katika sera zake je ni Israeli au Palestina? Je nani yuko sawa kiimani kati ya wayahudi na wakatoliki na sisi kama waafrika ama watanzania tuko upande gani? Nadhani ni wakati mwafaka kwetu sisi kuwa na muongozo kuhusu maswala haya muhimu katika sera za kidunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment