KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, May 17, 2009

China na Tetemeko la ardhi







China taifa kubwa linaloinuka kibiashara, kijeshi na kiuchumi duniani wiki hii lilikuwa linatimiza mwaka mmoja katika maombelezo ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi mwezi kama huu mwaka jana. Tetemeko hili liliweza kutoa mtihani wa jinsi gani taifa hili kubwa linaweza kupambana na majanga makubwa ya kidunia, huku vyomba vya Habari vya mataifa ya ulaya na marekani vikiwa vinaripoti khali mbaya katika maswala ya uokoaji na kuilamu china kwamba inaficha idadi kamili na ukubwa wa janga hilo china ilikuwa inajipanga kikamilifu katika kuokoa maisha ya maelfu ya watu waliokumbwa na tetemeko hilo.
Huku nchi kama marekani ikisahau janga la Katrina na jinsi Uongozi wa raisi bush ulivyoshindwa kutoa msaada wa kutosha kwa waliokumbwa na mafuriko huko kwao, hakuna taifa lolote lilikuwa linaikosoa katika swala la jinsi linavyofanya uokoaji huo. Mwaka mmoja sasa tangu janga hilo litokee china taifa hilo limejipanga vizuri na kurejesha matumaini kwa wananchi wake.
Pia liliwaadhibu vikali wahusika wote waliojenga majengo yaliokuwa chini ya kiwango na kusababisha maafa makubwa zaidi. Nchi hii imetoa mfano wa jinsi gani ya kujipanga na kutatua matatizo makubwa ya kidunia bila kutegemea misaada ya nje na kwetu ni changamoto tosha.
Tunawapa pole sana waathirika wote waliokumbwa na matatizo haya na tunawafariji wote waliopoteza Ndugu na mali zao na hata kupata ulemavu katika janga hilo.

No comments:

Post a Comment