KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, May 17, 2009

Raisi Obama agoma kutoa picha za mateso ya wafungwa

























































Happy to have them remain in Iraq


US hails approval of Iraq military accord


Referendum on Iraq security deal next year could c































Military doctors allegedly collaborated in prison torture





Raisi Obama agoma kutoa picha za mateso ya wafungwa
Katika khali ya kutotimiza ahadi yake, hivi karibuni Raisi kipenzi cha wengi Mr Barack Hussein Obama amegoma kuruhusu zoezi la kutoa picha zinazoonesha mateso waliyopata wafungwa wa kiiraki walipokuwa chini ya magereza yaliyokuwa yanasimamiwa na wanajeshi wa Kimarekani. Moja kati ya magereza hayo ni Abu Ghaib ambalo lilikuwa limekubuhu katika maswala ya mateso ya watuhumiwa wa ukhalifu mbalimbali. Kwa picha zilizowahi kutoka ndani ya shirika la upelelezi la marekani zilikuwa tosha kabisa kuonyesha khali halisi ya matendo yasiyo ya kibinadamu waliyofanyiwa wafungwa hao.

Akiingia madarakani kwa karata ya uwazi na ukweli huku akiapa kuwa tofauti na Uongozi uliotoka madarakani katika maswala ya Uongozi unaojali haki na uhuru wa wanadamu, kauli yake inapishana kabisa na ahadi hiyo.

Akitoa hoja ya kuwa picha hizo zinaweza kuleta khaliya chuki kwa wanajeshi wa kimarekani na kusababisha kupungua kwa usalama wa wanajeshi hao anasahau mambo makuu matatu ya kimaisha, kwanza likiwa kujiheshimu kama mwanadamu pili likiwa kuwaheshimu wanadamu wenzako na la mwisho likiwa uwajibikaji wa matendo yetu. Kwa picha hii unaweza kuona swala la uwajibikaji likikwepeshwa kwa kuwa taifa la watenda maovu hayo ni taifa lenye nguvu kubwa kiushawishi hapa duniani kwetu. Sidhani kama kuna taifa linaloweza kukamata raia wa kimarekani na kuwafunga na kuwatesa na kugoma kutoa maelezo yoyote kuhusu watu hao. Kama ikitokea khali hiyo nadhani dunia itajua kuwa mabwana nguvu hawa wana nguvu gani!

Kwa muelekeo huu Mr Obama ametuangusha wapenda haki wa dunia hii na kutufanya tuwe na hofu na hatima ya mbeleni ambazo anaweza kuchukua ukizingatia kuwa amerithi vita viwili huko iraki na afiganistani pia akiwa na wakati mgumu kiuchumi. Sisi wapenda amani wa maishani tunapenda kumsihi kiongozi huyu mpendwa aweke wazi maovu yote ya Uongozi uliopita na si kuchagua baadhi ya mambo na kuacha mengine, kumbuka aliweza kutoa maelezo ya mateso ya wafungwa wa gereza ya guantanamo liliopo cuba.
Kwa usemi wa ukweli utakuweka huru daima haina budi Mr yes We can kufanya hivyo kwa ajili ya mastakabali wa dunia yetu hii nzuri na yenye kuhitaji amani.

No comments:

Post a Comment