KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, May 24, 2009

11 wafariki katika tamasha Morocco






Watu wasiopungua 11 inaarifiwa wamefariki katika mji mkuu wa Rabat nchini Morocco na wengine 40 kujeruhiwa baada ya kukanyagana katika tamasha ya muziki ya Mawazine.









Watu wasiopungua 11 wamefariki katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, baada ya kukanyagana katika tamasha ya kimataifa ya muziki ya Mawazine.
Kulingana na waandishi habari, inadhaniwa kwamba watu wengine 40 walijeruhiwa baada ya uzio wa senyenge kuporomoka.

Tukio hilo lilifanyika usiku wa Jumamosi, wakati zaidi ya watu 70,000 walijaa pomoni katika uwanja wa michezo wa Hay Nahda, kumtizama mwanamuziki wa Morocco, Abdelaziz Stati.

Katika tamasha mwaka huu walioshiriki ni pamoja na Kylie Minogue, Khaled na Alicia Keyes.

Wadadisi wanasema kwamba tamasha hiyo ya wiki moja ya Mawazine ni kati ya mipango ya Morocco ya kuimarisha sifa nzuri za nchi hiyo ili taifa hilo lionekana ulimwenguni kwamba linakwenda sambamba na maendeleo ya kisasa.

Kulingana na maafisa wa polisi, wanawake watano, wanaume wanne, na watoto wawili, ndio waliofariki kati hali hiyo ya mkanyagano.

No comments:

Post a Comment