KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Sunday, May 24, 2009
Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini ajiua
Raia wa Korea Kusini wameonyesha kushtushwa sana na kifo cha ghafla cha rais wao wa zamani Roh Moo-hyun, aliyejiua baada ya kusakamwa kwa tuhuma za rushwa.
Raia wa Korea Kusini wameonyesha kushtushwa sana na kifo cha ghafla cha rais wao wa zamani Roh Moo-hyun, aliyejiua baada ya kusakamwa kwa tuhuma za rushwa.
Bwana Roh, aliyekuwa na umri wa miaka 62, alikufa baada ya kuanguka kutoka mlimani karibu na nyumba yake. Msemaji wake amesema aliacha waraka mfupi unaoelezea anajiua.
Rais Lee Myung-bak amesema anashindwa kuamini taarifa za kifo hicho na ni masikitiko makubwa. Mwezi uliopita Bwana Roh aliomba radhi kutokana na tuhuma za familia yake ilichukua rushwa ya dola milioni 6 wakati alipokuwa madarakani baina ya mwaka 2003-2008, lakini kamwe hakukiri kufanya jambo lolote kinyume na sheria.
Kiongozi huyo wa zamani ametokea katika familia isiyo na makuu, lakini alipanda ngazi hadi nafasi ya urais kutokana na usafi uliooneshwa na serikali na maridhiano yaliyofanywa na Korea Kaskazini.
Mwili wa Bwana Roh ulichukuliwa kwa msafara kutoka hospitalini katika mji wa kusini wa Busan siku ya Jumamosi mchana hadi katika mji alikozaliwa wa Gimhae, ambapo wasaidizi wake wamesema ndipo atakapozikwa.
Mamia ya askari polisi wakiwa katika sare zao pamoja na waombolezaji wengine walijipanga barabarani wakati mwili wake ulipokuwa ukisafirishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment