Katika matukio ya kufedhehesha mwaka huu ni tukio la maandamano ya wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki ambao waliandamana kutaka kulipwa mafao yao! Nguvu ilitumika kuwazuia ila kwa njia waliweza kutumia njia waliyoona inafaa kwao ili kuonyesha hasira na majonzi yao ya kuachwa solemba na serikali yetu! Huku wanasiasa wakisunda mabilioni ya shillingi hawa wakina mama na baba walikuwa wakizungushwa bila huruma yoyote! Ila sijui hawa wazee wetu kama walilipwa mafao yao ya uzeeni ama wamepigwa mkwara ama fiksi kali! Kwa mdau yoyote anayejua hatma ya hawa wazee wetu tafadhali tumeni tujulishane!
No comments:
Post a Comment