KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, April 4, 2009

Kila Jambo Maishani







IKIWA KILA JAMBO KATIKA MAISHA YETU SISI BINAADAMU LINA MWANZO NA MWISHO, KIPI KIFANYIKE ILI UTULIVU NA AMANI VIPATIKANE KATIKA NYOYO ZETU? KILA KUKICHA DUNIANI KUNA MAFURIKO, VIFOVYA KILA AINA,VITA AU MAPINDUZI YA NCHI, RUSHWA, UFISADI, BIASHARA YA VIUNGO VYA BINAADAMU, BIASHARA YA NGONO, MTU MME AU MKE WA MTU KUFUMANIWA , PESA ZA YATIMA NDIO MITAJI YA BAADHI YA WATU,HALI YA HEWA INABADILIKA KILA KUKICHA,UKIMWI NAO UNA KASI ZA AJABU, FITNA NA LAWAMA NDIO CHOMBO CHA RIZIKI KWA BAADHI YA WATU, UKITETEA HAKI YAKO UNAONEKANA UNAMSIMAMO MKALI ,VIFO VYA WASIO NA HATIA VIMEZOELEKA KATIKA NYOYO ZA KILA BINAADAMU.

KILA KUKICHA MATATIZO YANAONGEZEKA. NAJIULIZA HUU NDIO MWISHO WA DUNIA AU HUYU SHETANI ANA NGUVU KIASI GANI?

KWENYE IBAADA (MISIKITINI NA MAKANISANI) WATU WANAPUNGUWA KILA KUKICHA. VITUO VYA WATOTO YATIMA VINAZIDI KUFURIKA MACHOZI NA MACHUNGU NDIO JENGO LAO. HAWANA RAHA YA KUMWITA BABA AU MAMA KAMA WATOTO WENGINE. DUNIA HII INAELEKEA WAPI? MASIKIONI TUNASIKIA NA KUONA BAADHI YA WATU WAKITAJA BAADHI YA NCHI KUBWA DUNIANI KWAMBA NI VIONGOZI WA NCHI ZOTE DUNIANI. NA WENGINE WAKIITA AFRIKA KWAMBA NI BARA MASIKINI!
INAKUWAJE, BARA NDIO MASIKINI? UA WANANCHI NDIO MASIKINI?

MUNGU ANAJUA ZAIDI, NASI TUONGEZE BIDII YA ELIMU ILI TUWEZE KUA NA UFAHAMU USIOKUWA WA USHABIKI BALI WA MAENDELEO. KILA KIUMBE KATIKA DUNIA HII KINA RIZIKI YAKE, LAKINI KUNA BAADHI YA WATU AMBAO WANATUMIA NJIA YA KUMWAGA DAMU, DHULMA, RUSHWA,RIBA……n.k ) ILI WAWEZE KUFIKIA LENGO LA MAISHA BORA YA NAFSI ZAO. JAMBO HILO NI JAMBO AMBALO LINAWAUMIZA WATU WANYONGE ( MASIKINI ) KUPITA KIASI.

KWA WALE AMBAO WANAAMINI KUWEPO KWA MUNGU, NI JUU YAO KUVUMILIA NA KUTUMIA JITIHADA ZAO KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA HAKI INA SIMAMA KWA NJIA YA MAWAIDHA NA VITENDO. IKIWA WACHA MUNGU WATAHOFIA KUKEMEA MARADHI HAYO, KITAKACHOTOKEA NI MARADHI KUTAWALA DUNIA. KILA MTU ANAELEWA MACHUNGU YA MARADHI MWILINI MWAKE, NA NDIVYO MACHUNGU YATAKAVYO TAWALA KATIKA KILA NYOYO ZA WACHA MUNGU DUNIANI, BILA WAO KUTAMBUA KWAMBA NDIO WALIOFUGA UGONJWA HUO, MPAKA UMEWEZA KUWAMILIKI BILA KUJITAMBUA.




No comments:

Post a Comment