Je mwajua shughuli zetu za kila siku tangu tuamkapo mpaka tunaporudi kulala tunachangia kuchafua mazingira yetu kwa khali kubwa sana! ebu tafakari, umeamka unawasha simu yako, unawasha jiko lako, unawsha friji yako, unawasha tv yako, unawasha gari yako, unapanda basi au treni,unasoma gazeti yote hayo ni maangamizi ya mazingira yetu kwani kwa njia moja ama nyingine shughuli hizi hutoa joto la kaboni ambalo huchafua mazingira kwa khali ya juu kabisa, serekari zinanunua magari kibao, silaha kibao, watu wanafungua makampuni makubwa yanayochochea uzalishaji wa gesi chafu je kwa pamoja tunafanya juhudi gani ili kuokoa mazingira yetu? Kila kukicha nchi tajiri wanaonglea kupunguza uzalishaji wa gesi za joto kali je waathirika wakuu ni nani sisi maskini ama hao matajiri wakubwa ambao kila kukicha wanazalisha mabilioni ya hewa chafu? kwa ujumla sisi waafrika ni waathirika wakuu wa uchafuzi wa mazingira kwani ukame na joto kali vinatuathiri na miundombinu yetu ni dhaifu kupambana na khali hizo! je tufanyaje ili tujiokoe sisi na vizazi vyetu vijavyo! wote kwa pamoja tupigane kuweka mazingira yetu katika khali nzuri bila kutegemea nchi za ulaya,marekani na asia.nchi hizo ndizo chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira kutokana na juhudi zao za kutengeneza mabilioni ya pesa huku africa tukisumbuliwa na malaria,mlo umoja kwa siku,ukimwi,vita,ubovu wa malezi ........n.k
huu ni mda wa viongozi wa afrika kukubali kuwa kitu kimoja na kujali afya za waafrica wenzao bila kuweka maslahi yao mbele.
No comments:
Post a Comment