KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, April 7, 2009

Kondomu na Mambo yake




Wadau wenzangu nadhani wote tunajua matumizi ya mipira au condoms! ila hatujui habari za sehemu ambazo bidhaa hii ni adimu! Hapo ndipo utakapojua kuwa maishani kuna mambo! Wenzetu huzisafisha na kuzianika hizo bidhaa adimu kama dagaa ili ziweze kutumiwa tena kwa mara nyingine! Je hii ni njia salama! Je watu hawa wanaweza kusaidiwaje ukizingatia kuwa mabilioni ya pesa yanatolewa kwa ajili ya kujilinda na gonjwa la ukimwi ambalo linaweza kudhibitiwa kwa kuwa waaminifu na kujiepusha na zinaa ama kuvaa hiki kitu! Alafu kuhusu swala la elimu ya matumizi ya hiki kitu bila kujali umri wa mlengwa unaleta maswali ya ajabu! je watoto wana kondomu zao? kwani elimu hii inafundishwa mpaka shule za msingi! hivi hii si hatari kweli! kisha hivi matumizi ya kondomu na maadalili ya dini na jamii vinaingiliana? Alafu kwakuwa kondomu inatengenezwa kwa plastiki je vipi madhara yake kwa mazingira? na je tunafanyaje kulinda mazingira yetu na uchafuzi huu! vipi kuhusu maadili ya matangazo haya kwa familia kwani tangazo la kawaida la kondomu ni utata mtupu kwa familia yenye maadili kwani huonyesha machocheo ya zinaa kwa khali ya juu!Na mwisho inakuwaje kuwe kuna mfarakano kati ya hawa watengenazaji wa kondomu na miongozo yote ya kiimani? kwani watu hawa wa dini hupinga kabisa dhana ya matumizi ya kondomu! au ni kwasababu zinaa haina nafasi katika dini na maadili ya jamii? na hii ndio maana vijana wengi wanajiingiza katika zinaa na kusahau kabisa maadili ya dini na jamii! maana hata ndoa halali zimepungua wa na watu wanachukuana na kuachana kila kukicha? matokeo ya mambo haya yote yanotokana na wazazi kutoangalia mambo yanayochangia zinaa kama mavazi na matamanio mengine mengi na wanabakia kuhimiza kutumia kondomu kama kinga tu!hapo zamani gesti zilikuwa ni kwa ajili ya wageni na sasa ni tofauiti kabisa, kwa sasa zimekuwa viwanja vya ngono! je zahama hili la ukimwi litaisha kwa njia hii? leteni maoni yenu wadau!

No comments:

Post a Comment