KIFO NI MTENGANO AU KUTENGANA KWA ROHO NA MWILI.
ILI BINAADAMU AWEZE KUWEPO , LAZIMA KUWEPO VITU VIKUU VIWILI NAVYO NI MWANAMKE NA MWANA MUME.ISIPOKUWA KUNA BINAADAMU AMBAO WALIUMBWA,BILA BABA NA MAMA.BINAADAMU AMBAO
WALIUMBWA BILA MAMA NA BABA NI ADAMU NA HAWA.BINAADAMU MWINGINE ALIEZALIWA BILA KUWEPO NA BABA NI YESU ( ISA ).
KILA KITU HAPA DUNIANI, KINA MWANZO NA MWISHO NA NDIO MAANA BINADAMU HUZALIWA NA KUISHI KWA MDA HAPA DUNIANI NA MWISHO WA UHAI WAKE ( BINAADAMU ) HUWA NIWAHUZUNI NAWENYE MAUMIVU MAKALI. ILI BINADAMU AWEPO LAZIMA MWANAMKE NA MWANAMUME WAFANYE TENDO LA NDOA ( NDOA NI MKATABA BAINA YA MKE NA MUME NA NI USHAHIDI KWA NDUGU , JAMAA NA MARAFIKI, WA KWAMBA MKE NA MME HAO KUANZIA SASA WANAISHI KIHALALI).
MWANAMUME KAZI YAKE NI KUPELEKA MBEGU YA UHAI ( MANII ) NDANI YA MWANAMKE ( MWANAMKE KUKUBALI KUHIFADHI MBEGU YA
MWANAMUME ) .MBEGU HIO HUKAA NDANI YA MWANAMKE,NAKUANZA KUUMBIKA.MBEGU HUANZA KUWA KIPANDE CHA DAMU, KISHA HUWA KIPANDE CHA NYAMA KINACHOUMBIKA. KIUMBE HICHO KINAPOFIKIA MDA WA MIEZI MINNE,HUINGIZWA ROHO NDANI YAKE ( KWA WANAWAKE
WAJAWAZITO WANAPOFIKIA MWEZI WA NNE WA MIMBA,HUHISI MTOTO AKICHEZA TUMBONI ) HIO NDIO DALILI YA MTOTO ( BINADAMU ) KUPEWA ROHO. MUUNGANO WA ROHO NA MWILI,UNATENGENEZA KITUFULANI KINACHOITWA NAFSI. NAFSI NI MUUNGANO WA MWILI NA ROHO.
BINAADAMU ANAPOFARIKI AU KUFA, NDIO ISHARA YA KUTENGANA KWA ROHO NA MWILI.KINACHOMUUMIZA BINADAMU ANAPOONDOKEWA NA ROHO NI MAUMIVU YANAYOTOKANA NA MATENDO,MANENO,MILIKI…..N.K.
ROHO KUINGIA MWILINI NI RAHISI,KWASABABU MTU HAIHISI IKIINGIA..LAKINI MTU ANAHISI MAUMIVU YA HALI YA JUU KUTOKANA NA KUONDOKA ( KUTENGANA KWA ROHO NA MWILI ) KWA ROHO MWILINI.
ROHO INAPOMUINGIA MTU ( BINADAMU ) HUWA HAINA KITU ( HUWA TUPU ) LAKINI
INAPOONDOKA HUWA NA HIFADHI YA KUMBU KUMBU ZA MAISHA YAKE YA DUNIANI.
MUUMBA WA BINADAMU ( MUNGU ) ALIUMBA KILAKITU AKAKIPA MUONGOZO ( NJIA ),BINADAMU ANAWEZA KUUKUBALI AU KUUKATA , LAKINI MWISHO WA YOTE ROHO YAKE INARUDI KWA MUUMBA WAKE IKIWA NA RIPOTI NZIMA YA MAISHA YA MPITO YA DUNIANI.BINADAMU AKIFA KILA KITU ( PESA,MKE,WATOTO,BABA,MAMA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WOTE WANABAKI KATIKA HALI YAMASIKITIKO TU WALA HAWANA LOLOTE LA KUMSAIDIA LABDA MAOMBI TU.) KINABAKI DUNIANI.ANAONDOKA NA MATENDO YAKE TU,NDIO YATAKAYO MUHUKUMU ( KUMWEKA MAHALA PAZURI ) SIKU YA MALIPO AU SIKU YA KIAMA. NILAZIMA KILA ROHO IONDOKE NA MZIGO WAKE
QURAN :
KILA NAFSI ITAONJA MAUTI, NA TUNAKUFANYIENI MITIHANI KWA ( MAMBO YA ) SHARI NA KHERI , NA KWETU
( NYO TE ) MTAREJESHWA. ( 21 : 35 )
SIKU WATAKAYOWAONA MALAIKA HAITAKUWA FURAHA SIKU HIYO KWA WENYE MAKOSA, ( ITAKUWA NDIO SIKU YA KUTOLEWA ROHO ZAO ) NA WATASEMA ( SIKU HIYO ); “ MUNGU ) ATUEPUSHE MBALI ADHABU HII ILIYOTUKABILI.” ( LAKINI HAITAFAA KITU DUA HIYO ). ( 25 : 22 )
WATU WAPEPONI SIKU HIYO WATAKUWA KATIKA MAKAZI MEMA NA MAHARI PENYE STAREHE NJEMA.
BIBLE :
MSISTAAJABIE MANENO HAYO; KWA MAANA SAA YAJA,AMBAYO WATU WOTE WALIOMO MAKABURINI WATASIKIA SAUTI YAKE.NAO WATATOKA; WALE WALIOFANYA MEMA KWA UFUFUO WA HUKUMU. MIMI SIWEZI KUFANYA NENO MWENYEWE,KAMA NISIKIAVYO NDIVYO NIHUKUMUVYO NA HUKUMUYANGU NIYA HAKI, KWA SABABU SIYATAFUTI MAPENZI YANGU, BALI MAPENZI YAKE ALIYENIPELEKA. ( YOHANA MTAKATIFU 5 : 28,29,30 )
HII NI USHAHIDI WA VITABU VYA WATU WENYE IMANI YA KUWEPO KWA MUNGU. KILA NAFSI ITAKUFA,NA ITAULIZWA MATENDO YAKE YA HAPA DUNIANI. IKIWA WEWE NI MTU MWEMA UTALIPWA MEMA NA IKIWA NI MBAYA WA MATENDO UTALIPWA MABAYA.
EWE MUNGU WA MBINGU NA ARDHI TUNAKUOMBA UTUONGOZE KATIKA MATENDO MEMA NA UTUPE MAPUMZIKO MAZURI. AMIN
No comments:
Post a Comment