Mama ni kiungo muhimu katika maisha ya kila mwanadamu. licha ya kuwa kuna watu ambao katika historia zao hawana Mama kwa mfano Baba yetu Adamu Na Mama yetu Hawa, hao hawana baba wala mama. Lakini kwetu sisi tuliobaki, hatuna budi ya kumshukuru Mungu kwa kutuleta hapa duniani kupitia njia ya Mama.
Mama ni mzazi wa mtu kama mimi au wewe. Mama zetu wana majukumu makubwa yanayotokana na harakati za kuchukuwa mimba na kukaa nayo kwa muda wa miezi tisa. Kitendo hicho ni kitendo ambacho kinahitaji uvumilivu kutokana nashida zake za kimwili. Sio jambo zuri kwa mtoto kuwa mbishi juu ya mama yake. Mama alipata shida nyingi, juu ya mambo ya kujifungua na malezi kwa ujumla. Kila mzazi huwa makini katika malezi ya mwanae, na kuhakikisha kwamba anamlinda na kila jambo baya na kumpa kila zuri.
Wazazi kama binaadamu wanaweza kumkosea mtoto wao bila kujua, au wakijuwa kinachoendelea .Jambo la msingi juu ya mtoto husika ni kukubali matokeo na kuweza kuongea na wazazi wake bila ya jeuri. Si jambo la busara juu ya mtoto kutumia maneno ya jeuri juu ya mzazi wake ,kwasababu kitendo hicho kinasababisha machungu ndani ya nafsi ya mzazi husika. Machungu hayo yanatokana na mzazi kuvuta hisia za shida alizozipata katika malezi yako. Uchungu wa mzazi ni pigo la kiuchumi na kitabia juu ya mtoto husika. Mzazi ni mzazi hata kama utafanyaje, atabaki kuwa mzazi wako tu. Ndio maana mzazi wako anapoondoka duniani ( kifo ),huwezi kumpata mwanamke mwingine ambaye atachukuwa cheo cha mama yako na upole na upendo uliokuwa ukiupata juu yake. Kitakacho baki ni ukiulizwa kama una mama, jibu lako litakuja kama ifuatavyo nalo ni Sina Mama.
Ni vyema kumwonyesha mama upendo na kuwa karibu naye katika kila nyanja kabla ya kifo chake. Kifo cha mzazi ni pigo kubwa na ni vyema aondoke duniani kukiwepo uhusiano mzuri baina ya Mama na mwanae.
Mama ni nguzo ya maisha ya mtoto na Baba ni msingi wa maisha ya mtoto.
Mungu tupe moyo wenye nafuu ya mapenzi baina yetu na Wazazi wetu.

No comments:
Post a Comment