KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, April 4, 2009

JOSEPH KONY NA BENDERA YA DAMU


Joseph Kony
Huyo ndiye Joseph Kony wa Uganda! Jamaa ni bwana vita ambaye anadai ametumwa na Mungu afanye nchi ya Uganda Itawaliwe na Amri kumi za Mungu anazozijua yeye! Kwani keshaua watoto, mama, baba, babu, bibi, kuchoma nyumba, mashamba, shule, mahospitali, kutia watu ulemavu wa kudumu, kubaka na kuchoma watu visu, yaani jamaa ana masoho mpaka ibilisi mwenyewe hathubu kujilinganisha naye! Huyu ni mwafrika mwenzetu aliyezaliwa na mama na baba wa kiafrika ila amekuwa janga na balaa kwa maisha ya waafrika kibao! Hivi sasa anaishi kama digidigi huko kwenye misitu ya kongo na sudani pia haamini mtu yoyote wa karibu yake anafanya uchawi kila kukicha! Hivi kwanini watu kama hawa ambao wanaua watu na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu na kupoteza rasilimali na kuvuruga miundombinu na kunyima watu fursa za kujiendeleza na kuishi kwa amani wanapewa nafasi eti nao wawe viongozi wa watu haohao waliowafanyia maasi hayo pia hupelekwa kwenye mahakama za chipsi kuku huko hague kisha mashtaka yao huchukua miaka kuisha? Watu kama hawa hukumu yao ni panga! Ukiuwa kwa upanga utakufa kwa upanga! Mungu kwako ndiokuna hukumu ya ukweli hapa kwetu hasa afrika ni wizi mtupuuuu! Maskini tunaangamizwa na wanasiasa kwa jina la demokrasia! Huku tukijifunika mahema, kunywa maji ya mito na kula mahindi ya nguruwe kutoka USA na wala si kutoka kwa waafrika wenzetu wanaoweza kutoonea huruma kweli tumekosa heshima kwetu na kwa waafrika wenzetu huku wenye raha wakiimba afrika iungane! Hivi ni vituko na wazimu vya khali ya juu! Kony hafai kuunganisha nyoyo katika jina la amri za mwenyezi mungu kwa sababu moja ya amri hizo inasema usiuwe na yeye ndio kawaida yake kutoa nyoyo za watu bila woga wowote! Wadau leteni maoni yenu ili tuikomboe afrika yetu!

No comments:

Post a Comment