KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, April 4, 2009

MWANGA WA NAFSI







MWANGA WA NAFSI,NI KITENDO AMBACHO KINASABABISHWA NA UKOMAVU WA AKILI.
KAMA TUNAVYOJUA KILA MTU ANA ROHO NA KILA ROHO INAMFUMO WAKE WA KIMAISHA.
ROHO HUBADILIKA PALE AMBAPO, INAKUTANA NA MWILI.
MUUNGANO WA MWILI NA ROHO,UNATENGENEZA KITU AMBACHO KINAITWA NAFSI.
KAWAIDA YA NAFSI,INAPENDA VITU VIZURI NA INACHUKIA VITU VIBAYA.
NAFSI INA MTINDO,WA KUTUMIA KIGEZO CHA KUPENDA AU KUCHUKIA JAMBO FULANI.
NAFSI INAPENDA KUPITIA NJIA ,YA MAWASILIANO YA KIPEKE. NAFSI HUJENGA MAPENZI AU CHUKI KUTOKANA NA MASLAHI YAKE JUU YA JAMBO FULANI.BAADHI YA NJIA AMBAZO ZINAIFANYA NAFSI IJENGE CHUKI AU MAPENZI NI KAMA :

1 ) MACHO : MACHO NI CHOMBO AMBACHO,KINAIWEZESHA NAFSI KUANGALIA JAMBO ( KITENDO,RANGI,SURA,UMBULE……n.k ) FULANI.

2) PUA : PUA NI MOJAWAPO WA KIFAA KINACHOWEZESHA NAFSI KUPENDA AU KUCHUKIA HARUFU FULANI.

3) MDOMO : MDOMO NI KIFAA AMBACHO KINAIWEZESHA NAFSI KUPENDA
( LADHA YA KINYWAJI AU CHAKULA AU MANENO YA SAUTI ) JAMBO FULANI.

4 ) MASIKIO : MASIKIO NI VIFAA,AMBAVYO VINAIFANYA NAFSI IWEZE KUPENDA AU KUCHUKIA SAUTI NA MANENO FULANI.

5 ) MOYO : MOYO NI KIFAA, AMBACHO KINA KAZI NYINGI NDANI YA MWILI WABINAADAMU,MOJAWAPO NI KAZI YA DAMU NA KUHIFADHI KUMBU KUMBU ZA NAFSI. MOYO UNA TABIA YA PENDA YULE ANAEPENDA NAFSI YAKE NA KUCHUKIA YULE ANAYECHUKIA NAFSI YAKE.

KILA BINAADAMU ANA UWEZO WA KUWA NA MAADUI WENGI ZAIDI YA MARAFIKI. KITENDO HICHO KINAWEZA KUTOKANA NA KILA NAFSI KULINDA MASLAHI YAKE BILA KUJALI MADHARA YA MASLAHI HUSIKA.

MWANGA WA NAFSI NI USTARABU ULIOMO NDANI YA NAFSI HUSIKA.KUMBUKA KWAMBA USTARABU,HAUPATIKANI BILA YA ELIMU

No comments:

Post a Comment