Unajua muziki ni burudani! Inaelimisha na kuburudisha vyote kwa pamoja ila muziki wa sasa umejaa vibweka kwani ni zaidi ya burudani kama ilivyokuwa hapo nyuma. Ebu cheki hizi picha hapo ili upate japo mwangaza kidogo, ukiwaona hao wadada kutoka Uganda utajiuliza? Je ile burudani na elimu ni nguo zao walizo vaa? Ama ujumbe wa nyimbozao! Ama hivyo vibweka wanavyofanya! Kisha wacheki wadada wa Akudo walivyopindishwa migongo utadhani ni walemavu! Wanakuburudisha na kukuelimisha nini na pozi hilo? Mbona hao wakaka wamepozi poa tu? Kisha ona hiyo mipasuo ya suruali zao! Jamani ndugu zangu upofu huu utatupeleka pabaya! Ebu leteni michango yenu ili tuweze kuweka haya mambo ya burudani na elimu kwa njia ya muziki sawa!
No comments:
Post a Comment