KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, April 4, 2009

BAADHI YA MASHUJA WA AFRICA


Hawa ni baadhi ya mashujaa wetu!Wadau ebu jikumbushe viongozi wetu hao shupavu, walipigania uhuru wa nchi zetu kwa nguvu zao zote, wengine waligeuka kuwa waangamizi wan chi hizo walizotawala mmoja wao ni mobutu seseseko wazabanga aliyegeuza Zaire kuwa dimbwi la umasikini licha ya maliasili na madini yote Mwenyezi Mungu alizowajalia! Yupo pia Mfalme Haile Selais Mungu wa Majah people aliye uawa kinyama na Mengistu Mariam na kumzika katika choo cha kasri ya ikulu yao, yupo pia Baba yetu wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye kwa nguvu zote alipiga vita rushwa na ubadhirifu katika Tanzania na Afrika kwa ujumla aliyengatuka kwa ridhaa yake binafsi! Mungu awalaze wote wasio kuwepo nasi na awajalie baraka tele kwa mema waliyotenda kwa bara letu la Afrika! Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment