Mashindano ya Kombe la Dunia na hali ya kuyumba kwa uchumi ni mambo yaliyosababisha kujumuishwa kwa maneno mapya katika kamusi ya Kiingereza ya Oxford (Oxford Dictionary of English).
Vuvuzela, ni neno jipya, likiwa na maana ya chombo cha kupulizwa kilichotumiwa na mashabiki wa soka wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
Vile vile matatizo ya uchumi duniani yameongeza "toxic debt" - deni lenye uwezekano wa kutolipwa.
Kamusi hiyo - tofauti na nyingine ijulikanayo kama Oxford English Dictionary (OED) ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 - ina maneno mapya zaidi ya 2,000.
Inakusudia kuainisha mambo ya kisasa katika matumizi ya lugha ya kiingereza.
Toleo lake la tatu lilihusisha maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
No comments:
Post a Comment