KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 19, 2010

Majeshi ya Marekani yaondoka Iraq

Kikosi cha mapigano cha jeshi la Marekani kilichokuwa cha mwisho kusalia nchini Iraq kinaondoka, ikiwa ni wiki mbili kabla ya ratiba iliyowekwa awali.

Kikosi hicho cha nne cha askari wa miguu, kinaondoka kufuatia sera ya Rais Obama ya kumaliza shughuli za mapigano nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Majeshi hayo yamekuwa yakiondoka nchini humo kupitia nchi jirani ya Kuwait.

Hata hivyo takriban wanajeshi elfu hamsini na sita wa Marekani watasalia nchini humo sio kwa shughuli za kivita mbali kuwezesha amani na kutumika chini ya amri ya serikali ya Iraq. Wanatakiwa pia kujikinga wakati wa mashambulizi.

Msemaji wa wizara ya masuala ya kigeni wa Marekani amesema kuwa marekani baado itaendeela kuisaidi Iraq ili iweze kupata uthabiti na amani. Pamoja na hayo itaweka kumbukumbu ya majeshi ya Marekani elfu nne waliuawa vitani.



























No comments:

Post a Comment