KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, July 1, 2010
Amuua Baba Yake Kwa Kufanya Kazi na Wamarekani
Kijana mmoja nchini Iraq amemuua baba yake mzazi kwa kumpiga risasi baada ya baba yake kukataa kuacha kazi yake kama mkalimani wa wanajeshi wa Marekani.
Kijana huyo alimpiga risasi ya kifua baba yake wakati alipokuwa amelala baada ya baba yake huyo kupinga kuiacha kazi yake kama mkalimani wa jeshi la Marekani.
Tukio hilo lilitokea siku ya ijumaa ambayo pia watu 27 walifariki nchini Iraq kufuatia mashambulizi ya mabomu kwenye nyumba za maafisa wa serikali na majeshi ya serikali ya Iraq.
Hameed al-Daraji, 50, alikuwa akifanya kazi kama mkalimani wa majeshi ya Marekani kwa miaka saba kuanzia mwaka 2003 ambapo majeshi ya Marekani yalifanikiwa kumng'oa aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein.
Hameed alipigwa risasi ya kifua kwenye majira ya saa tisa usiku, alipokuwa amelala kwenye nyumba yake iliyopo kwenye mji wa Samarra.
Taarifa ya polisi ilisema kuwa Hameed aliuliwa na mwanae ambaye alitaka kuthibitisha uamifu wake kwa wanamgambo wa Al-Qaida ambao alijiunga nao hivi karibuni.
Polisi walisema kuwa kijana aliyetiwa mbaroni ni Abdul-Halim Hameed, 30, ambaye awali mwaka 2007 alitangaza kuachana na mtandao wa ugaidi baada ya majeshi ya Marekani kuzidisha mashambulizi yake.
Alijiunga tena na mtandao huo hivi karibuni na alimuua baba yake ambaye alimuona kama adui anayewasaidia Wamarekani.
Polisi wanamshikilia Abdul-Halim pamoja na binamu yake inaaminika alimshirikisha katika mauaji hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment