KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, June 29, 2010
Mtoto afia ndani wakati mama yake amekwenda kununua chips
MTOTO wa kike wa miaka minne amefariki dunia kwa kuzidiwa na moshi na moto uliosababishwa na mshumaa wakati mama yake alipotoka kwenda kunumnua chips na kumfungia mtoto huyo ndani.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea siku mbili zilizopita huko maeneo ya Vingunguti kwa Simba jijini Dar es Salaam majira ya usiku.
Ilidaiwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa, mama huyo alikuwa akiongea na wapangaji wenzake nje ya nyumba hiyo na hatimaye waliachana ilipofika saa 4 na kila mmoja aliingia ndani kwake kwa ajili ya kulala.
Walidai kuwa mama huyo bila kuwataarifu wenzake mtoto wake alipolala alimlaza na kumfungia ndani na kisha yeye kutoka bila kuwataarifu wenzake.
Kwa kuwa nyumba yao hiyo haina umeme walikuwa wakitumia mishumaa na taa nyingine za ziada, ndipo mama huyo alipoamua kuwasha mshumaa na kuuweka mezani na kisha kufunga mlango kwa kuwa mwanae alilala na yeye kutoka kwenda kununua chips bila kutoa taarifa kwa wenzake.
Hivyo haikufahamika mara moja kama mshumaa huo uliangushwa na panya, ama upepo, hivyo uliweza kuanguka na kuunguza vitu vya ndani humo kidogokidogo na mtoto huyo kuanza kuathirika na moshi uliozagaa ndani humo na hakuweza kujisaidia kwa kuwa mlango ulifungwa na alipopiga kelele watu hawakumsikia kwa kuwa walikuwa walishaanza kulala.
Ilidaiwa kuwa wanaume waliokuwa katika banda la nje waliokuwa wakiangalia mpira waliona moshi ukitoka ndani humo na kwenda kuwaamsha wenye nyumba na kuwaambia nyumba inaungua ndipo walipogundua na kuamka na kuanza kumwita mama huyo bila ya jibu lolote kutoka chumbani humo.
BIla kutambua kama mtoto alikuwa ndani humo watu hao walifanya juhudi za hapa na pale kuzima moto na baadae walipoingia ndani walimkuta mtoto huyo yupo katika hali mbaya na kumkibmiza hospitalini.
Ndani ya chumba hicho hakuna kitu ambacho kilipona viliteketea kwa moto vyote.
Wakati watu wakiwa katika hatua za mwisho za uzimaji moto na mtoto ameshakimbizwa hospitalini mama huyo ndipo alipokuwa akirudi akiwa na chips zake mkononi na kukuta hali hiyo na ghafla alipoteza fahamu papohapo.
Mtoto huyo aliweza kupoteza maisha dakika chache wakati amefishwa hospitali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment