KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Matatani kwa jaribio la kumrubuni mwanafunzi


KIJANA mmoja [jina tunalo] amejikuta akipewa notisi kwenye nyumba aliyokuwa amepanga baada ya kukutwa akiwa katika jaribio la kumrubuni mtoto wa mwenye nyumba aliyokuwa amepanga huko Manzese jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo alikutwa na binti huyo wa miaka 15 anayesoma kidato cha kwanza akiwa amekaa nae baa katika jaribio la kumrubuni mwanafunzi huyo.

Bila kutambua lolote mjomba wa binti huyo alimuona kijana huyo akiwa anaingia nae baa huko maeneo ya Sinza Mori na kuanza kufanya nae mazungumzo ya hapa na pale huku mjomba huyo akiwa katika kona moja nzuri akiwaangalia wawili hao.

Kwa kuwa mjomba huyo nae alikuwa na machungu ya kutaka mpwa wake huyo apate elimu alipatwa na hasira za ghafla za kutaka amvamie binti huyo lakini wawili aliokuwa amekaa nao mahali hapo walimpoza na kumuamuru amuangalie kwanza.

Kijana huyo bila kutambua lolote alimuagizia chakula binti huyo na huku yeye akiendelea na kinywaji na kisha kuendelea na mazungumzo ya hapa na pale na binti huyo.

Mjomba huyo uzalendo ukamshinda aliinuka na kwenda kwenye meza waliyokuwa wamekaa wawili hao na kumshika binti yake na kumuuliza alikuwa akifanya nini mahali hapo?

Binti huyo alianza kuangua kilio mahali hapo kabla hajaanza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na kumuomba radhi mjomba wake huyo.

Mjomba huyo alikodi usafiri aina ya tax na kwenda nae hadi nyumbani kwa dada yake na kuanza kumuuliza alikuwa akifanya mazungumzo yepi na kijana huyo.

Ndipo binti huyo alipowaeleza ukweli kuwa alikuwa akimwambia kuwa anamuhitaji katika maisha na alimueleza kuwa amalize masomo ili amuoe.

Kabla hajamaliza maelezo yake mama yake alianza kumpa kichapo cha nguvu huku akisaidiwa na kaka yake huyo kwa kukubali kwenda nae baa huku akijua yeye ni mwanafunzi.

Hivyo wazazi hao walikerwa na kitendo cha kijana huyo kutaka kumuaribia masomo binti yao walimsubiri kijana huyo arudi nyumbani kwao hapo na bila mafanikio siku hiyo kijana huyo hakurudi kwa kuwa aliona hali ya hewa ilishaaribika.

Siku ya pili majira ya usiku wa saa tano kijana huyo alirudi nyumbani kwake hapo na alipoonekana walimdaka na kumpeleka kituoni ili akatoe maelezo na kupewa notisi hiyo huko.

No comments:

Post a Comment