KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, June 21, 2010

Mimba na uzazi

TAYO
Mimba inaweza kutungwa iwapo mwanamke au msichana aliyekaribu umri wa kupata hedhi, ama anaepata hedhi, atafanya ngono na mwanamme, pasi na kutumia mbinu yoyote ya kuzuia mimba.
La kusikitisha ni kwamba hilo linaweza kumtokea hata msichana mdogo aliye na umri wa miaka 9 au 10.

Kwa hivyo elimu ya afya ya uzazi ni muhimu zaidi kwa kundi hili la vijana. Kwani nao wavulana pale wanapoanza kusisimka kimapenzi, wanaweza kutoa manii au shahawa ambazo zina mbegu za uzazi. Mbegu hizo zina uwezo wa kutunga mimba.

Hii ni kumaanisha wavulana, hata wakiwa kwenye miaka ya kumi na kuendelea, wanaweza kumtunga msichana au mwanamke mimba!

Jinsi Mimba inavyotungwa

Ili mwanamke kuingia katika majira yake ya hedhi, mwili wake huangua yai kila mwezi, kutoka sehemu ya kiungo cha uzazi kinachoitwa ovari. Yai hili huteremka polepole kupitia mirija ya ovari likisafiri kwa mda wa siku 8 hadi 12 kuelekea nyumba ya uzazi.

Wakati mwanaume anapotoa manii (pale anapofanya ngono na mwanamke), manii hayo huwa yamebeba mamilioni ya mbegu za kiume, ila moja tu inapokutana na yai la mwanamke, inatosha kumtunga mimba.

Kwa hivyo kama mwanamke atafanya ngono na mbegu ya mwanamme ilifikie yai, mimba inaweza kutungwa. Kisha mbegu hizo zilizotangamana na kuwa kitu kimoja (mimba), zitajipachika kwenye nyumba ya uzazi, ambapo zitapata virutubisho vya kuikuza mimba hiyo.

Lakini kama mimba haikutungwa basi mwanamke huyo atapata hedhi kama kawaida.

Baada ya hivyo nini hufanyika?

Muungano huo wa yai na mbegu ya mwanamme, ambao sasa ni mimba, hukua.

Matiti ya mwanamke mwenye mimba hunawiri na kuongezeka ukubwa ishara ya kujitayarisha kutoa maziwa ya kumnyonyesha mtoto pindi atakapozaliwa.

Watoto wengi huzaliwa miezi tisa baada ya mimba kutunga.

Uzazi

Wakati mtoto anapokuwa tayari kuzaliwa, misuli ya mfuko wa uzazi, huanza kujikunja na kujikunjua, hali ambayo huifanya misuli ya uke wa uzazi pia kutanuka. Huu ndio mwanzo wa uchungu wa uzazi.

Inapofikia wakati fulani maji maji ambayo huwa yanamemhifadhi mtoto ndani ya tumbo la mama huanza kutoka yakipitia ukeni. Huku kunaitwa 'kuvunja chupa' na maji hayo yanaweza kutoka kwa nguvu ama pole pole.

Na ndio njia hii hii ambayo mtoto pia hatimae atapitia wakati wa kuzaliwa.

Kila jinsi kasi ya misuli inavyojikunja na kujinyosha ndivyo maumivu ya uchungu yanavyoongezeka, na polepole huifanya shingo ya mfuko wa uzazi kufunguka. Wakati ikifunguka na kufikia sentimita 10, mwanamke hupatwa na hisia za kama kusukuma kitu.

Kila anavyosukuma, mtoto nae hupenya na hatimae kutoka – kupitia ukeni (kwa kawaida kichwa ndicho kinachotangulia kutoka). Punde mtoto akizaliwa huandamana na kilio cha uchangani hali inayomwezesha kufungua njia za kuvutia pumzi.

Pindi mtoto akizaliwa, mrija wa kitovu hukatwa. Kiungo hiki ndicho kilichokuwa kikisafirisha virutubisho vyengine kutoka kwa mama hadi kwa mtoto ndani ya mimba. Vitovu matumboni mwetu ndiyo alama tunayobaki nayo.

Nao mfuko wa uzazi (ambao ulikuwa ukimhifadhi mtoto wakati wote wa miezi tisa tumboni) hutoka vilevile kupitia ukeni.

Utajiepusha vipi kupata mimba?

Usisadiki ngano, na hadithi unazozisikia mitaani kuhusu kuzuia mimba.

Ukweli ni kwamba unaweza kupata mimba hata ile mara ya kwanza tu utakayofanya mapenzi. Ukweli ni kwamba unaweza kupata mimba katika mtindo wowote utakaotumia kufanya ngono, ama namna yoyote utakavyokuwa umelala au umesimama. (Baadhi ya watu hudhani wakifanya mapenzi kusimama hawatapata mimba!)

Na unaweza kupata mimba hata ukiwa na hedhi, ama kufanya mapenzi ndani ya maji!

Njia bora zaidi ya kuzuia mimba, ni kutofanya mapenzi kabisa au kutumia mbinu ya kuzuia mimba kila unapofanya mapenzi. (Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu za kuzuia mimba na njia za mpango wa uzazi kwa jumla

No comments:

Post a Comment