Umoja wa Mataifa umesema wanajeshi wanne wa kulinda amani raia wa Afrika Kusini, waliotekwa nyara katika jimbo la Darfur nchini Sudan mapema mwezi huu wameachiliwa huru.
Wanajeshi hao wanahudumu katika kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kilichoko mjini Nyala, Kusini mwa Darfur. Msemaji wa watekaji nyara hao, Ibrahim al Dukki, amesema kundi la Movement for Popular Struggle, lilihusika na utekaji nyara huo na ameongeza kuwa hawakulipwa kikombozi ili kuwaachilia huru wanajeshi hao.
Al Dukki amesema wanajeshi hao walitekwa nyara ili kuonyesha hali ya usalama katika jimbo hilo la Darfur halikuruhusu zoezi la uchaguzi mkuu kufanyika katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment