KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, April 27, 2010

Sudan yasherehekea ushindi wa rais Bashir

Rais wa Sudan, Omar al Bashir ameongoza sherehe za kuchaguliwa kwake tena kama rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kwa zaidi ya miongo miwili.

Chama tawala cha National Congress Party, NCP, kimesema ushindi wa rais Al Bashir unakemea mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, iliyokuwa imetoa kibali cha kukamatwa kwake kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.

Katika eneo la Kusini, Makamu wa rais wa kwanza wa Sudan na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kirr Mayardit, alishinda kiti cha Urais katika eneo la Kusini kwa idadi kubwa ya kura. Uchaguzi huo sasa umetoa fursa nzuri ya kuandaliwa kwa kura ya maoni mwaka ujao kuhusu uhuru wa eneo la Kusini.

No comments:

Post a Comment