KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, March 3, 2010

Marekani kupunguza silaha za nuclear


Rais Barack Obama ameanzisha utaratibu unaonuwia kupunguza silaha za nuclear zinazomilikiwa na Marekani.
Bw Obama alikutana na waziri wake wa ulinzi, Robert Gates, kujadili mkakati mpya, ambao maafisa wanasema utakuwa muhimu katika mpango wa rais wa kutaka kuufanya ulimwengu kuwa mahali salama pasipo kuwa na silaha za nuclear.


Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na suala hilo.

Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema Rais Obama anatarajiwa kufutilia mbali mipango ya kuendeleza silaha mpya za nuclear.

Wakati huo huo, suala moja lingine muhimu linabakia--ambalo ni lini silaha za nuclear zinaweza kutumika.

No comments:

Post a Comment