Marekani imesema shughuli ya kuwahamisha watu waliojeruhiwa vibaya wakati wa tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti itaanza upya saa chache zijazo.
Msemaji wa Ikulu ya White House Tommy Vietor, amesema serikali ya Marekani imeshirikiana na washirika wake wa kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na utawala wa majimbo yote nchini humo kuongeza viwango vya kuwahudumia wagonjwa kutoka Haiti.
Safari za ndege kutoka Haiti zilisitishwa siku ya jumatano na madaktari wengi nchini humo wanahofia kuwa wagonjwa wengi huenda wakafariki.
Bwana Vietor amekanusha kuwa tatizo hilo lilisababishwa na ukosefu wa pesa, akisema kwamba safari za ndege zilisitishwa kutokana na hitilafu za utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa wagonjwa hao
No comments:
Post a Comment