Kundi la kutetea haki za binadamu Nigeria limeisihi mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuchunguza ghasia baina ya wasialmu na wakristo katika mji wa Jos.
Kundi hilo liitwalo Serap, limemwandikia mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno-Ocampo wakimwomba achunguze vifo vya watu 326 katika ghasia hizo.
Wanaharakati hao wanataka jeshi na polisi zichunguzwe kwa madai ya kutumia nguvu nyingi katika kutuliza ghasia.
Waislamu na Wakristo walipigana kwa siku kadhaa mwezi Januari.
Idadi rasmi iliyotolewa na polisi ni vifo 326, huku waislmu wakisema ni 364.
Viongozi wa kikristo hawajathibitisha idadi ya waliokufa, ijapokuwa makadirio ya awali ni wakristo 65.
No comments:
Post a Comment