KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Obama ahuzunishwa na mauwaji ya Fort Hood





Rais wa marekani Barack Obama amesema "hakuna imani ya dini inayotetea" mauwaji ya wiki iliyopita ya watu 13 katika kambi ya jeshi Texas.
Bwana Obama alitoa matamshi hayo wakati akihutubia watu katika ibada ya mazishi ya wale waliouwawa huko Fort Hood, baada ya kukutana na jamaa za waliofariki.

Meja Nidal Malik Hasan, anayeshutumiwa kwa mauwaji hayo,alipigwa risasi na polisi na bado yuko hospitali.

Idara ya ujasusi ya marekani ilifahamu kama Meja Hasan alikuwa akiwasiliana na kiongozi mmoja wa dini anayeunga mkono al-Qaeda.

Bwana Obama alisema waombolezaji wamekuja "kutoa heshima zao kwa wanaume na wanawake 13 walioshindwa kuepuka jinamizi la vita,hata wakiwa katika mazingira tulivu ya nyumbani".

No comments:

Post a Comment