Mfanyakazi wa kifaransa atekwa Chad
Mfanyakazi wa kifaransa wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu, ICRC ametekwa na watu wenye silaha mashariki mwa Chad.
Shirika hilo la ICRC limesema linasimamisha shughuli zake kwa muda katika eneo hilo.
Limesema mfanyakazi wake, Laurent Maurice, alitekwa mapema Jumatatu katika kijiji cha Kawa, takriban kilomita 20 kutoka mpaka wa Sudan.
Shirika hilo limesema halijui watekaji nyara hao ni akina nani na wana nia ipi.
No comments:
Post a Comment