KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 2, 2009

Biashara ya almasi zimbabwe ikomeshwe


Zimbabwe inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa ifurushwe kutoka kwenye biashara ya kimataifa ya almasi kufuatia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wanajeshi wake.
Halmashauri ya kimataifa inayosimamia biashara hiyo, 'Kimberly Process' imetakiwa na wanaharakati wa haki za kibinadamu kukomesha Zimbabwe kuuza almasi.

Kilio hiki kimejitokeza kufuatia tuhuma dhidi ya wanajeshi wa nchi hiyo kuwatesa raia. Kwa mujibu wa wakereketwa wa haki za binadamu, wanajeshi wamewaua takriban watu miambili katika migodi ya almasi, ingawa serikali imekanusha madai hayo.

Halmashauri hiyo yenye wanachama sabini, iliundwa mwaka wa 2003, kwa minajili ya kuwahakikishia wateja wa bidhaa hiyo kwamba Almasi wanayonunua haitumiki kufadhili vita au ukiukwaji wa haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment