KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 20, 2009

Usain Bolt atunukiwa heshima ya taifa


Usain Bolt atunukiwa heshima ya taifa

Mwanariadha bingwa wa mbio fupi za mita 100 duniani Usain Bolt wa Jamaica, ametunukiwa nishani kuu ya kutukuka ya Jamaica iitwayo, The Order of Jamaica.
Kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye medani ya riadha kwa kiwango cha kimataifa, Usain Bolt ametunukiwa nishani hiyo na Gavana Mkuu wa Jamaica Ptrick Allen katika makazi ya Gavana ya King's House mjini Kingstone.

Bolt akiwa amevalia suti yake nadhifu akiwa mtu mwenye umri mdogo kutunukiwa nishani hiyo nchini Jamaica, alipanda jukwani kupokea nishani hiyo huku akishangiliwa na wageni waalikwa.

Hata hivyo wapo walioonesha mashaka kukabidhiwa Bolt nishani hiyo kwa madai kawaida hupewa wale waliotumikia nchi kwa muda mrefu.


Hata hivyo Waziri Mkuu wa Jamaica Bruce Golding akijibu madai hayo amesema huenda itakuwa vigumu kwa Bolt kuweza kufanikiwa zaidi atakapofikisha umri mkubwa kwenye riadha tofauti na alivyofanikiwa sasa.

Bolt alikuwa mwanadamu wa kwanza katika historia ya michezo ya Olympic kuvunja rekodi ya mbio za mita 100 na 200 katika michezo iliyofanyika Beijing China na akaweka rekodi mpya ya dunia ya mita 100 mjini Berlin ya sekunde 9.58 na pia rekodi ya mbio za mita 200 ya sekunde 19.19.

No comments:

Post a Comment