KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, October 20, 2009
Hakuna zawadi kwa kiongozi wa Afrika
Mfanyabiashara mkubwa wa Sudan Mo Ibrahim mwaka huu hakutoa zawadi ya utawala bora ya dola milioni 5 kwa kiongozi mstaafu wa Afrika.
Bw Ibrahim hakutoa sababu kwa uamuzi wake huo lakini akasema katika mikakati yao wamezingatia katika baadhi ya miaka hakutakuwa na mshindi.
Huu ni mwaka wa tatu wa kutolewa zawadi kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara, aliyetumikia muda wake na kuukamilisha kwa njia ya kidemokrasia.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na John Kufuor wa Ghana walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda zawadi hiyo.
Mshindi anajinyakulia dola milioni tano kwa kipindi cha miaka 10 na baadae dola 200,000 kwa mwaka kwa kipindi chote cha maisha yake, ikiwa ni zawadi kubwa kupewa mtu mmoja duniani.
Bw Ibrahim amesema watu wataamua wenyewe kwa nini hakuna mshindi aliyepatiwa zawadi hiyo mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment