KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, June 5, 2009
Utabibu kwenye ndege
Utabibu kwenye ndege
Ndege moja ya kipekee imewasili mjini Nairobi, kutoa matibabu ya macho kwa wagonjwa maskini. Upasuaji huo unafanyika ndani ya ndege ambayo pia ni hospitali.
Ndege moja ya kipekee imewasili mjini Nairobi, kutoa matibabu ya macho kwa wagonjwa maskini pamoja na mafunzo kwa wakufunzi wa udaktari.
Kwa muda wa wiki mbili wataalamu wa macho wa shirika la kimataifa la misaada la Orbis International.
Wangonjwa hao watafanyiwa upasuaji ndani ya ndege hiyo, ambayo pia ni hospitali. Kwa kawaida unapokwenda katika uwanja wa ndege huwa ni kwa nia ya kusafiri au kupokea mgeni wako ambaye amewasili kutoka safarini.
Lakini baadhi ya familia zenye watoto wenye magonjwa ya macho walipata fursa ya matibabu ya bure katika ndege isiyo ya kawaida, ndege iliyogeuzwa kuwa hospitali ya matiabbu ya magonjwa ya macho. Ni hospitali kama nyingine tu, ila imo ndani ya ndege.
Ina vifaa vya hali ya juu vinavyopatikana katika hospitali za kimataifa. Maabara, chumba cha upasuaji, vyumba vya wagonjwa na zaidi ya hayo kuna darasa la mafunzo kwa wakufunzi arobaini na nane wa udaktari.
Ndege hii inayomilikiwa na shirika la Orbis International hutua katika mataifa mbalimbali kote duniani lakini hasa mataifa yasiyo na uwezo wa kutoa huduma bora za afya ambapo wagonjwa wengi pia hawawezi kugharamia huduma za kitaalamu za matibabu.
Niliitembelea ndege hiyo siku ambapo huduma zake zilikuwa zinaanza kutolewa. Wagonjwa waliokuwa wamefika walikuwa wamechaguliwa kwa ushirikiano wa shirika hilo na hospitali kubwa zaidi ya kitaifa ya Kenyatta pamoja na hospitali ya matibabu ya macho ya Kikuyu ili karibu na mji wa Nairobi.
Nilipoingia ndani ya ndege, kilichonichonivutia kwanza ni darasa lililokuwa na wanafunzi arobaini na nane ambao walikuwa wakifuatilia katika runinga kubwa upasuaji ambao ulikuwa unaendelea katika chumba cha upasuaji.
" Kwa sasa mafunzo yanaendelea na tunahakikisha mafunzo haya yatawawezesha wakufunzi kuendesha matibabu katika hali yoyote" anasema Jack Rivers ambaye ni afisa mkuu wa shirika la Orbis International.
Baada ya hapo chumba kinachofuata ni kile cha upasuaji wa Leser na hapo pia wagonjwa walikuwa wakisubiri kufanyiwa upasuaji. Wagonjwa wengi walikuwa wamekuja kutoka katika maeneo ya mbali kama vile mkoa wa kati na pwani ya Kenya. Mmoja wao ni Ashley Faraja mwenye umri wa miaka kumi. Alikuwa amefika na mamake kufanyiwa upasuaji. Jicho lake lilikuwa limefura na limekuwa hivyo tangu alipokuwa mchanga.
Mamake Ashley, Mary Atieno alipata wakati mgumu kumtafutia mwanawe matibabu hadi alipobahatika kuwa miongoni mwa waliochaguliwa kupokea matibabu ya bure katika ndege hii. Hospitali hii itawahudumia wagonjwa kama Ashley kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuondoka. Ndege hii imetoa huduma hizi katika mataifa sabini na nane yakiwemo Ethiopia na Sudan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment