KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 4, 2009

Marekani yalaumu China kuhusu vifo Tiananmen







Waziri wa mambo ya nje Bi Hillary Clinton
Miaka 20 imepita tangu maelfu ya waandamanaji kuuawa na vikosi vya serikali kwenye mnara wa Tiananmen nchini Uchina.
Mamia ya watu wangali kizuizini tangu wakamatwe kwa kuhusika katika maandamano hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hilary Clinton ameitaka serikali ya Uchina kuwajibika kuhusu mauaji hayo, kuwaachilia huru na kukoma kuwatesa wale walioshiriki katika maandamano hayo.

Tukio hilo ni nyeti mno nchini Uchina kiasi kwamba hairuhusiwi kujadiliwa hadharani.

Tayari ulinzi mkali umewekwa jijini Beijing.

Wapinzani wengi wamekuwa wakishinikizwa kuondoka jijini Beijing au wanazuiliwa katika nyumba zao.

Hivyo ndivyo hali ilivyo hata kwa wapinzani wanaoishi katika sehemu kama vile Hong Kong ambako watu wana uhuru wa kujieleza.

Hata hivyo Bi Clinton alisema wakati huu wa kuadhimisha miaka 20 ya kisa hicho ni fursa nzuri kwa Uchina kutafakari na kuchunguza kwa makini maovu yake ya siku zilizopita na kutoa hesabu kamili ya watu waliouawa, waliofungwa au hawajulikani waliko, kama moja wapo wa njia za kujirekebisha na kuleta maridhiano.

“Uchina inaweza kuonyesha heshima yake kwa matukio ya siku hiyo kwa kutoa kipa umbele kwa jitihada za kudumisha utawala wa kisheria, kulinda haki za binadamu na kukuza demokrasia kama vile inavyoendeleza mabadiliko katika mfumo wake wa kiuchumi”, alisema Bi Clinton.

No comments:

Post a Comment